Klabu ya FC Porto imetangaza rasmi kumsajili kiungo wa kimataifa wa Korea Kusini, Hwang In-beom, kutoka Feyenoord ya Uholanzi. Kiungo huyo amesaini mkataba wa miaka mitatu utakaodumu hadi Juni 2029, ukiwa na chaguo la kuongeza mwaka mmoja zaidi. Porto imelipa euro milioni 4.5 kwa ajili ya usajili huo, huku ada hiyo ikitarajiwa kuongezeka kwa euro 500,000 kulingana na mafanikio ya mchezaji huyo.
Hwang, ambaye alicheza misimu miwili akiwa Feyenoord baada ya kujiunga kutoka Crvena Zvezda ya Serbia, aliwasili jijini Porto mwishoni mwa wiki, akafanyiwa vipimo vya afya na kutambulishwa rasmi Jumatatu. Kiungo huyo anatarajiwa kuziba nafasi iliyoachwa na Seko Fofana, aliyemaliza kipindi chake cha mkopo katika klabu hiyo mwishoni mwa msimu uliopita.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
“Nina furaha kubwa kusaini FC Porto, moja ya klabu bora duniani. Ni heshima kubwa kuichezea klabu hii na kuuwakilisha mji huu. Mimi na familia yangu tuliwahi kutembelea Porto, na mke wangu alipenda zaidi mji huu kuliko Lisbon. Nimejiandaa kwa changamoto hii mpya na naamini tunaweza kufanya jambo la kipekee msimu huu,” alisema Hwang baada ya kutambulishwa.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 29 pia alizungumza kuhusu aina ya uchezaji wake, akisema: “Mimi ni mchezaji ambaye hutoa kila kitu uwanjani hata ninapokuwa nimechoka. Kila mara nataka kuvuka mipaka yangu kwenye mazoezi na mechi. Natumaini mtazamo huu utatimiza matarajio ya mashabiki, na siwezi kusubiri kucheza mbele yao.”
Hwang In-beom aliiwakilisha Korea Kusini katika michuano ya Dunia 2026 na msimu uliopita alicheza mechi 24 akiwa Feyenoord, akifunga bao moja na kutoa pasi nne za mabao. Akiwa na uzoefu wa kucheza Rubin Kazan, Olympiacos, Crvena Zvezda na Feyenoord, pamoja na mechi 77 na mabao saba kwa timu ya taifa, Porto inaamini kiungo huyo atakuwa nyongeza muhimu katika kikosi chake kuelekea msimu mpya.


