Kiungo wa Chelsea, Enzo Fernandez, amesema kwa mara ya kwanza kuwa hafikirii kuhusu mustakabali wake wa klabu kwa sasa, licha ya kuendelea kuhusishwa na tetesi za kuhamia Real Madrid katika dirisha lijalo la usajili.
Akizungumza baada ya kuisaidia Argentina kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Misri na kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya Dunia, Fernandez alisema akili yake yote imeelekezwa kwenye mashindano hayo. “Kwa sasa ninajikita kikamilifu na mashindano ya Dunia. Baada ya mashindano kumalizika ndipo nitakapofikiria kuhusu mambo mengine,” alisema kiungo huyo.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kauli hiyo imekuja kufuatia tamko la wakala wake aliyedokeza kuwa mchezaji huyo anaweza kuondoka Chelsea, huku akieleza kuwa Real Madrid ingekuwa moja ya chaguo bora kwa mustakabali wake. Hata hivyo, klabu hiyo ya Hispania imekanusha kuhusika na mazungumzo yoyote ya usajili wa Fernandez.
Katika taarifa yake, Real Madrid ilisisitiza kuwa, “Tunaiheshimu Chelsea na hatuna mazungumzo wala mpango wa kumsajili Enzo Fernandez. Hatutaki kuhusishwa na taarifa zisizo sahihi zinazozunguka kwenye vyombo vya habari.”

Wakati huo huo, Chelsea inaendelea kushikilia msimamo wake kwamba haitamuuza nyota huyo kwa ada isiyopungua pauni milioni 120. Mbali na Real Madrid, Paris Saint-Germain pia imekuwa ikitajwa miongoni mwa vilabu vinavyofuatilia kwa karibu hali ya kiungo huyo wa Argentina, huku hatma yake ikitarajiwa kujulikana baada ya michuano ya Dunia kumalizika.


