Klabu ya Feyenoord imethibitisha usajili wa mlinda mlango Mjerumani Tjark Ernst kutoka Hertha BSC kwa mkataba wa miaka minne. Usajili huo umekuja baada ya kuonekana wazi kuwa nahodha wa Feyenoord, Timon Wellenreuther, ataondoka katika klabu hiyo na kujiunga na Wolfsburg.
Ernst mwenye umri wa miaka 23 alikuwa kwenye mazungumzo na Feyenoord kwa muda na makubaliano yalifikiwa mapema wiki hii kabla ya kutangazwa rasmi. Kipa huyo amesema amefurahia kujiunga na timu hiyo yenye historia kubwa nchini Uholanzi na inayoshiriki mashindano ya Ulaya mara kwa mara.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
“Ni jambo la kipekee sasa kuweza kujiita mchezaji wa Feyenoord. Tangu mazungumzo ya kwanza nilihisi kuwa huu ni uamuzi sahihi. Klabu hii ina malengo makubwa na hilo linaendana na matarajio yangu,” alisema Ernst kupitia tovuti rasmi ya klabu.
Kipa huyo alijiunga na Hertha BSC mwaka 2023 akitokea VfL Bochum na amecheza jumla ya mechi 93 akiwa na timu hiyo inayoshiriki daraja la pili nchini Ujerumani. Ernst anatarajiwa kuchukua nafasi ya kwanza ya ulinzi wa lango Feyenoord mbele ya Liam Bossin, huku klabu hiyo ikitarajiwa kutafuta kipa mwingine wa akiba. “Baada ya miaka mitatu katika Bundesliga 2, nahisi nimejiandaa kwa hatua hii mpya. Hii ni mara yangu ya kwanza kucheza nje ya Ujerumani, na nimejiunga na klabu kubwa inayoshiriki mashindano ya Ulaya kila msimu na itacheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao,” aliongeza Ernst.
Ernst pia ameeleza shauku yake ya kuanza rasmi maisha yake mapya Rotterdam, hasa tukio la siku ya utambulisho wa wachezaji wapya ambapo Feyenoord huwaingiza wachezaji uwanjani kwa helikopta mbele ya mashabiki wao. Kipa huyo amesema anasubiri kwa hamu kukutana na mashabiki katika uwanja wa De Kuip. “Siwezi kusubiri kusimama langoni katika De Kuip. Najua mechi za Ulaya hupokelewa kwa hisia kubwa sana hapa, na Feyenoord inajulikana kwa hilo si tu nchini Uholanzi bali pia barani Ulaya. Natamani siku ya kuingia uwanjani kwa helikopta na kukutana na mashabiki kwa mara ya kwanza,” alisema.
Feyenoord ambayo ilimuondoa kocha Robin van Persie baada ya msimu wa 2025/26 na kumteua tena Giovanni van Bronckhorst kuwa kocha mkuu, tayari imepata nafasi ya moja kwa moja katika hatua ya ligi ya UEFA Champions League. Timu hiyo itaanza kampeni yake ya Eredivisie msimu mpya tarehe 9 Agosti dhidi ya Sparta Rotterdam.


