Kocha wa Bayern Munich Hansi Flick anataka kuona mengi kutoka kwa mchezaji Leroy Sane lakini amesema mshambuliaji huyo anahitaji muda.

Tangu ajiunge na Bayern akitokea Manchester City kwa dau linaloripotiwa kuwa €45m mapema mwaka huuSane amefanikiwa kufunga magoli matano na kutoa asisti mbili katika michezo tisa.

Mshambuliaji huyo aliukosa karibia msimu wote 2019-20 akiwa Man City baada ya kuwa na jeraha la (ACL).

Wakati Flick akimtaka Sane aimarike lakini pia anajiandaa kuwa nasubira ya kupata huduma ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 baada ya kupata jeraha.

“Asilimia mia yupo sawa, ufanisi wake ni mkubwa,” aliongea na waandishi wa habari.

“Lakini kama ilivyokuwa kwa wachezaji wengine, alikuwa akipoteza mipira mara nyingi kwenye mchezo dhidi ya Salzburg, hakuonesha ile one on one kuna sababu na tayari tumeongea kuhusu hilo, ata jaribu kuwa bora zaidi mara nyingine.

“Kimsingi anahitaji muda hii ni baada ya kudumu na majeraha kwa muda mrefu na ataupata huo muda anafanya mazoezi kwa bidii sana.

Katika michezo sita ya Bundesliga mitatu kati hiyo alianza msimu huu na Sane amefunga magoli matatu na kutoa asisti mbili.

Pia ametengeneza nafasi kubwa nne, ni Thomas Muller pekee mwenye sita, Sege Gnabry, Admir Mehmedi na Raphel Guerreiro ambao wametengeneza nafasi kubwa tano wanao mzidi.


USICHELEWE KUKAMATA MKWANJA HUU!

Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.

Meridianbet Tanzania Casino

SOMA ZAIDI

19 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa