Flick Awahimiza Wachezaji wake Kuipa Kipaombele Derby, Licha YA Ligi ya Mabingwa

Kocha wa FC Barcelona, Hansi Flick, amewataka wachezaji wake kuelekeza nguvu zao kwenye mchezo wa derby ya La Liga dhidi ya Espanyol, licha ya kuwepo kwa presha ya mashindano ya UEFA Champions League.

Flick Awahimiza Wachezaji wake Kuipa Kipaombele Derby, Licha YA Ligi ya MabingwaKauli hiyo imekuja baada ya Barcelona kupoteza kwa mabao 2-0 dhidi ya Atletico Madrid katika mchezo wa kwanza wa robo fainali uliochezwa katikati ya wiki, matokeo yanayowalazimu kupambana vikali katika mchezo wa marudiano utakaochezwa jijini Madrid. Hata hivyo, Flick amesisitiza umuhimu wa mchezo wa ndani dhidi ya Espanyol.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Akizungumza na waandishi wa habari, Flick alisema “Ndoto ya kila mchezaji, klabu, mashabiki na makocha ni kushinda Ligi ya Mabingwa. Katika kila mchezo wa Ulaya unaona timu ikiwa na hamasa ya ziada.” Aliongeza: “Huu ni ushindani mkubwa, lakini tunapaswa kufanya kazi yetu ya kila siku katika La Liga.”

Flick Awahimiza Wachezaji wake Kuipa Kipaombele Derby, Licha YA Ligi ya MabingwaKocha huyo aliweka wazi kuwa licha ya kuipa thamani kubwa Ligi ya Mabingwa, bado wanahitaji umakini katika ligi ya ndani akisema “Mwisho wa siku jambo muhimu zaidi ni kushinda Ligi ya Mabingwa. Hilo ndilo lengo langu, la wachezaji na klabu.” Barcelona kwa sasa wanaongoza ligi kwa tofauti ya pointi saba dhidi ya Real Madrid.

Flick pia aligusia umuhimu wa derby hiyo, akisema “Tuna wachezaji wengi waliotoka La Masia, wanajua vizuri maana ya kucheza dhidi ya Espanyol. Ni derby, tunacheza nyumbani na ninataka kushinda.” Aliongeza kuwa atafanya mabadiliko ya kikosi ili kusimamia vyema nguvu za wachezaji kati ya mechi mbili dhidi ya Atletico.

Flick Awahimiza Wachezaji wake Kuipa Kipaombele Derby, Licha YA Ligi ya MabingwaAkihitimisha, Flick alisisitiza kuwa wachezaji wake hawatapoteza umakini kuelekea mchezo wa marudiano, akisema “Hii ni kazi yao. Wako makini sana na wako tayari kwa mchezo wa kesho.”

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.