Foden Apewa Mkataba Mpya Kusalia City

Manchester City wameanza mazungumzo ya awali na Phil Foden kuhusu mkataba mpya, hatua inayoonyesha klabu bado inamwona kama sehemu muhimu ya mradi wao wa muda mrefu. Hii inakuja licha ya kiungo huyo wa England kupungua muda wake wa kucheza chini ya Pep Guardiola msimu huu, jambo lililoibua maswali miongoni mwa mashabiki.

Foden Apewa Mkataba Mpya Kusalia City

Kwa mujibu wa The Times, City wamefungua mazungumzo ya mapema na mawakala wa Foden ili kuondoa sintofahamu kuhusu mustakabali wake. Ingawa mkataba wake wa sasa unaendelea hadi 2027, uongozi wa klabu unaona ni muhimu kumfunga mapema ili kuepuka hatari ya kumpoteza nyota wao.

Hali ya Foden uwanjani msimu huu imekuwa tofauti na alivyotarajiwa. Amejikuta akipoteza nafasi ya kuanza katika kikosi cha Guardiola, huku ushindani ndani ya timu ukiwa mkali zaidi kuliko kawaida. Hata hivyo, klabu bado inasisitiza kuwa anaitajika sana kwenye mipango yao ya muda mrefu.

Foden Apewa Mkataba Mpya Kusalia City

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Guardiola naye amekiri kuwa Foden anapitia kipindi cha changamoto, lakini akisisitiza kwamba mchezaji lazima apambane kupata nafasi yake. Maneno yake yanaonyesha wazi kwamba hakuna nafasi ya kudumu kwa jina lolote. Hii imeongeza presha lakini pia hamasa kwa nyota huyo kurejea kwenye kiwango chake bora.

Foden Apewa Mkataba Mpya Kusalia City

Wakati mazungumzo ya mkataba yakiendelea, klabu za Ulaya kama Barcelona na Bayern Munich zimekuwa zikifuatilia hali yake kwa ukaribu. Hata hivyo, City hawana mpango wa kumuuza. Foden sasa anatarajiwa kupigania nafasi yake tena, akianza na matumaini ya kurejea kikosi cha kwanza kwenye mechi dhidi ya Everton.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.