Phil Foden ameanza kurudisha makali yake kuelekea Kombe la Dunia baada ya kuonyesha kiwango bora katika ushindi wa Manchester City wa mabao 3-0 dhidi ya Crystal Palace. Na sasa, nguli wa zamani wa City Micah Richards ameibuka hadharani kumtetea nyota huyo akisisitiza kuwa England wanamuhitaji kwenye mashindano makubwa.

Foden alikuwa moto usiku huo baada ya kutoa pasi mbili za mabao, ikiwemo pasi ya kisigino iliyowashangaza wengi na kumtengenezea Antoine Semenyo bao la kwanza. Kiungo huyo alipokea mpira akiwa amegeuza mgongo golini kabla ya kutoa pasi ya akili kubwa iliyofungua kabisa safu ya Palace na kuonyesha ubora wake wa kipekee.
Richards amesema aina hiyo ya ubunifu ndiyo inayomfanya Foden kuwa tofauti na wachezaji wengine ndani ya kikosi cha England. Kwa mujibu wake, kwenye mechi ngumu ambapo timu pinzani zinajilinda kwa wingi, Foden ana uwezo wa kufungua mlango kwa pasi moja au nafasi moja pekee.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Ingawa Foden hajawa na msimu bora sana akiwa na mabao saba na assist tano Premier League, Richards anaamini uwezo wake wa kufikiria haraka na kucheza soka kwa akili ni kitu ambacho hakiwezi kupuuzwa na kocha Thomas Tuchel. Amesema hata kama nyota huyo hajang’aa sana msimu huu, bado ana kitu cha tofauti ndani yake.

Sasa macho yote yataelekezwa kwa Tuchel ambaye anatarajiwa kutangaza kikosi chake rasmi Mei 22. Je, Foden atapata nafasi ya kwenda Marekani na kuonyesha kiwango chake kwenye Kombe la Dunia, au kiwango chake cha msimu huu kitamgharimu? Mashabiki wa England tayari wameanza kugawanyika kuhusu mjadala huo mkubwa.


