Bondia Javier Fortuna amelezea kiu yake ya kutaka kumlambisha sakafu bondia machachari Ryan Garcia katika pambano lao lijalo ambalo limepangwa kufanyika siku ya Jumamosi katika ukumbi wa Crypto.com Arena huko Los Angeles.

Mwanamasumbwi huyo wa Kidomikana anaonyesha hataki kabisa kumuacha Ryan ashinde pambano hili kufuatia kuwa na kumbukumbu ya kupoteza katika pambano la raundi 12 kwa miaka ya hivi karibuni.

Fortuna anachokiamini ni kwamba alistahili kushinda mapambano yaliyopita dhidi ya Robert Easter Jr na Joseph Diaz Jr hivyo pambano na Garcia ni muhimu sana kwenye kazi yake hiyo.

Nitampiga kwa KO,” Fortuna aliiambia BoxingScene.com

“Siwezi kufika naye kwenye ubao wa matokeo, hata ikatokea nikamdondosha mara nyingi lakini kama tukifika kwenye uamuzi wa majaji siwezi kushinda hivyo njia pekee ya kushinda ni kumlaza chini.


BETI NGUMI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa