Kiungo wa klabu ya Barcelona Frenkie De Jong na timu ya taifa ya Uholanzi Frenkie De Jong amegeuka kua lulu ndani ya klabu ya Barcelona baada ya kuikataa klabu ya Manchester United katika dirisha kubwa lililopita.

Frenkie De Jong amekua moja ya wachezaji muhimu ndani ya klabu ya Barcelona chini ya kocha Xavi Hernandez tangu tu alipoikataa klabu ya Manchester United kwenye dirisha la usajili lililopita, Hii imemfanya mchezaji huyo kuibwa sana ndani ya klabu hiyo.frenkie de jongKocha Xavi Hernandez amenukuliw akimmwagia sifa kiungo huyo wa kimataifa wa Uholanzi na hiyo ni kutokana na ubora ambao amekua akiuonesha ndani ya klabu hiyo, Kiasi kwamba kocha Xavi amevutiwa nae sana tofauti na msimu ambao umemalizika.

Taarifa zilieleza mwanzoni kocha Xavi alipoingia ndani ya klabu ya Barcelona moja ya wachezaji ambao hawakua kipaumbele chake basi ni Frenkie De Jong, Lakini baada ya kugoma kuondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu uliomalizika amegeuka kua mchezaji muhimu zaidi kwenye kikosi cha Barca.frenkie de jongFrenkie De Jong leo atakua moja ya wachezaji ambao watakua wanaiongoza klabu ya Barcelona dhidi ya Manchester United katika dimba la Old Trafford kwenye mcherzo wa kombe la Uefa Europe League, Ikiwa ni uwanja ambao alihitajika zaidi kuucheza kama uwanja wake wa nyumbani alikataa.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa