MSHAMBULIAJI wa Arsenal anayefanya vizuri kwa sasa Gabriel Jesus, amekataa kumlaumu yeyote ila yeye mwenyewe baada ya kuachwa nje ya kikosi cha Brazil kwa ajili ya mechi zao mbili za kirafiki mwezi huu.

 

Gabriel Jesus:Naheshimu Sana Uamuzi wa Kocha.

Vijana wa Tite watamenyana na Ghana na Tunisia nchini Ufaransa wiki ijayo huku wakicheza mechi ya mwisho kwenye maandalizi yao ya Kombe la Dunia huko Qatar, ambayo ndio wanapewa nafasi kubwa kushinda.

Lakini mshambuliaji Jesus, pamoja na wachezaji wenzake wa Arsenal, Gabriel Martinelli na Gabriel Magalhaes, waliondolewa kwenye kikosi cha wachezaji 26 ambacho kina wachezaji 11 wa Ligi kuu ya Uingereza.

Hao ni pamoja na Roberto Firmino na Richarlison, ambao wanashindana na Jesus kwenye nafasi ya mshambuliaji wa kati wa timu ya Brazil.

 

Gabriel Jesus:Naheshimu Sana Uamuzi wa Kocha.

Kukosekana kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 kulishangaza kwani ameanza maisha mazuri ndani ya Arsenal kufuatia uhamisho wake wa pauni milioni 45 kutoka Manchester City majira ya kiangazi, akifunga mabao manne katika mechi nane.

Lakini Jesus ameapa kufanya kazi kwa bidii ili kushinda tena nafasi yake kwenye kikosi cha Kombe la Dunia, ambalo sasa limebakiza miezi miwili tu.

 

Gabriel Jesus:Naheshimu Sana Uamuzi wa Kocha.

“Kulikuwa na mawasiliano, baada ya kuitwa, ndio,” aliiambia ESPN Brasil. ‘Naheshimu sana uamuzi wa kocha, namheshimu Tite, wafanyakazi wote.

‘Kama nilivyosema, mimi ni Mbrazil, siku zote nitaiweka timu. Na pia ninawaheshimu wachezaji wengine, ambao wana ubora mwingi. Nitaendelea kufanya niwezavyo ili kupata fursa tena.

‘Kilicho katika udhibiti wangu ni utendaji wangu. Nitajaribu kila wakati kuwa bora, kumaliza michezo. Leo nilikuwa na nafasi ambazo ningeweza pia kuboresha zaidi kidogo, najua. Nimekuwa nikifanya mazoezi, nikijaribu kufanya bora yangu.’

Jesus amefunga mabao 19 katika mechi 56 alizoichezea Brazil, lakini amefunga mara moja pekee katika mechi zake 21 za kimataifa tangu kufunga kwenye fainali ya Copa America 2019 wakati nchi yake ilipoilaza Peru.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa