Klabu ya Galatasaray imekataa ofa ya euro milioni 60 (takribani Sh bilioni 182.84 za Kitanzania) kutoka Tottenham Hotspur kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wake nyota, Victor Osimhen, huku hatma ya mchezaji huyo ikiendelea kuzua mjadala katika dirisha la usajili la majira ya joto.
Kwa mujibu wa taarifa za Polymarket Sports, Osimhen bado anawindwa na klabu kadhaa barani Ulaya kutokana na kiwango bora alichoonyesha tangu alipojiunga na Galatasaray akitokea Napoli ya Italia.
mpira wa miguu, kubeti mpira wa miguu, bashiri soka, soka, beti kwenye soka, odds za soka, bashiri mpira wa miguu, beti za soka, beti mechi za soka, odds za kubeti mpira wa miguu
Hata hivyo, Galatasaray imeonyesha kutokuwa tayari kumuachia mshambuliaji huyo kwa kiwango hicho cha fedha, jambo linaloacha maswali iwapo Tottenham itawasilisha ofa mpya yenye thamani kubwa zaidi kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili.
Osimhen alikuwa mmoja wa nyota waliobeba mafanikio ya Galatasaray msimu uliopita, akiisaidia klabu hiyo kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Uturuki kwa mara ya pili mfululizo. Katika mechi 33 za mashindano yote, mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Nigeria alifunga mabao 22 na kutoa pasi nane za mabao, akithibitisha kuwa mmoja wa washambuliaji hatari zaidi barani Ulaya.
Iwapo mazungumzo yataendelea katika siku zijazo, Tottenham italazimika kuongeza dau lake ili kuwashawishi Galatasaray kumuuza nyota huyo, ambaye anaendelea kuwa miongoni mwa wachezaji wanaovutia zaidi katika soko la usajili la majira ya joto.


