Kocha mkuu wa Napoli Gennaro Gattuso bado haja anza kuelekeza mawazo yake kunako ligi ya Mabingwa Ulaya, ambako anamchezo wa marudiano dhidi ya timu ya Barcelona, anataka kumalizana kwanza na Serie A akiwa katika nafasi nzuri.

Napoli waliicharaza Roma 2-1 siku ya Jumapili nakukaa katika nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi, wakiwa na rekodi ya kushinda michezo minne kati ya mitano iliyopita.

Watakutana na Barca kwa mchezo wa marudiano nchini Ureno mwezi Agosti ikiwa mchezo wa kwanza walikwenda 1-1 Napoli akiwa katika dimba la nyubani mwezi Februari.

 

Gattuso ambaye kwa upande wake atakutana na Genoa siku ya Jumatano , amesema kwa sasa hakuna haja ya kuanza kujiandaa dhidi ya wababe hao wa LaLiga.

“Bado kuna muda,” alisema hayo baada mchezo wao na Roma kumalizika Napoli wakiwa wametoka kifua mbele kwa kuziweka kibindoni alama tatu.

Tuna mwezi mmoja mbele,lazima tufikirie kumaliza ligi tukiwa katika nafasi za juu na kuongeza nguvu kwenye miguu yetu . Ni swala fulani la kutumia akili Zaidi.

“Siku hizi nataka kuiweka vyema timu kwa sababu wachezaji wengi wataendelea kuwepo klabuni hapa tunahitaji kujenga akili ya kushinda.”

52 MAONI

  1. Gattuso amekuwa na kikosi imara kabisa ambacho kinaweza kumsaidia kufanya makubwa kwenye soka na kuingiza jina lake kwenye historia

  2. Ni super gattuso anacho sema kinaweza kikawa sie maana sio rahisi kusema nafikilia ligi ya mabingwa wakat bado ligi haijaisha lazima amalizane na serie A alafu aamishie akili zake uefa champions league

  3. Kiukweli ni lazima upambanie ligi ya ndani uhakikishe upo kwenye nafasi gani ya kushiriki ligi ya mabingwa msimu ujao kwa gatuso yuko sahihi kwa alicho kisema.

  4. Tuna mwezi mmoja mbele,lazima tufikirie kumaliza ligi tukiwa katika nafasi za juu na kuongeza nguvu kwenye miguu yetu . Ni swala fulani la kutumia akili Zaidi.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa