Mchezaji wa Barcelona Gavi amefunguka jinsi anavyoifurahia timu hiyo baada ya miamba hao wa Uhispania kufanya sajili nzuri na jinsi zitakavyo imarisha kikosi hicho baada ya kumaliza msimu uliyopita bila kikombe chochote.
Gavi ambaye anaingia msimu wake wa pili na Barca ya wakubwa baada ya kupandishwa na kocha Ronald Koeman ameelezea furaha yake kwa Barca mpya.
“Mimi ndiye mchezaji namba moja ninayefurahishwa na timu hii na watu wanapaswa kuifurahia pia,”alisema Gavi.
“Tumefanya usajili mzuri, na tayari wamecheza vyema tutumaini tutaendelea kama hivi.
Gavi hakuishia hapo alituma ujumbe kwa mashabiki wa Barca baada ya kuifunga Real Madrid kwa mabao 1-0 kwenye mchezo wa kirafiki wa Pre-Season huko Las Vegas.
“Ninawaomba wawe na uvumilivu, tutajitahidi kuwapa kile kilicho bora?