Steven Gerrad ambaye ni kocha mkuu wa klabu ya Aston Villa yupo katika wakati mgumu hivi sasa baada ya kuwa na mwendelezo mbaya wa matokeo ambayo anayapata katika ligi kuu ya Uingerezaa.

Ikumbukwe kuwa Steven Gerrad alijiunga na timu hiyo mwaka jana 2021 lakini  kabla hajajiunga na timu hiyo, ilikuwa chini ya kocha mkuu Dean Smith ambaye alitupiwa virago baada ya kuwa hana matokeo chanya ndani ya klabu.
Gerrad(42) Hajui XI Wake Bora

Gerrad ambaye ni mchezaji wa zamani wa Liverpool mpaka sasa katika mechi nne ambazo amecheza ameshinda mechi moja tuu ambayo nayo ni dhidi ya Everton lakini zote amepoteza hata ile ya kwanza ya kwenye ufunguzi wa ligi ambayo alicheza dhidi ya FC Bournemouth na kupoteza kwa mabao mawili kwa bila lakini pia na kupoteza mchezo mwingine wakiwa nyumbani dhidi ya Westham United kwa bao moja kwa bila.

Kutokana na mwendelezo wa kupoteza mechi kumefanya mchambuzi wa mpira wa Skysports kusema kuwa Steven Gerrad hajui kikosi chake cha kwanza ambacho kitakuwa kinaanza.Wamemnunua Philipe Coutinho lakini hawezi kucheza timu moja na Emi Buendia na hicho ndio kitu kikubwa kibaya alisema.

Gerrad(42) Hajui XI Wake Bora

Ni tatizo kubwa sana kama Gerrad  hajui kikosi cha kwanza baada ya mechi nne ambazo amecheza na anaenda kukubiliana na mechi mbili kubwa zijazo ambazo atacheza dhidi ya Arsenal vilevile dhidi ya Manchester City kitu ambacho asipoangalia atajikuta yupo katika timu tatu zinazoshika mkia.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa