Gharama za Kumfukuza Carrick Zaiweka Manchester United Kwenye Presha

Mustakabali wa kocha wa Manchester United, Michael Carrick, umeendelea kujadiliwa kufuatia mwanzo usioridhisha wa msimu wa 2026/27. United imepata matokeo yanayoweka presha kwenye benchi la ufundi, ikiwemo kutolewa kwenye Carabao Cup baada ya kufungwa 3-2 na Brighton katika Uwanja wa Old Trafford.

Gharama za Kumfukuza Carrick Zaiweka Manchester United Kwenye PreshaCarrick alipewa mkataba mpya wa kuendelea kuinoa United hadi mwaka 2028 baada ya kuiongoza timu hiyo kumaliza nafasi ya tatu msimu uliopita na kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya. Uongozi wa klabu uliamua kumuamini baada ya kipindi chake kizuri cha awali, huku taarifa rasmi za klabu zikisema alistahili kuendelea na nafasi hiyo.

Hata hivyo, gharama za kuvunja mkataba huo zimeibua mjadala mwingine. Mshauri wa zamani wa masuala ya fedha wa Manchester City, Stefan Borson, aliiambia Football Insider kwamba United inaweza kukabiliwa na gharama kubwa ikiwa itaamua kumfuta Carrick na kutafuta benchi jipya la ufundi. “Manchester United kuna uwezekano mkubwa isifanye uamuzi huo mapema kutokana na gharama zinazohusishwa,” Borson alisema.

Gharama za Kumfukuza Carrick Zaiweka Manchester United Kwenye PreshaLicha ya presha hiyo, Carrick mwenyewe amesema hajikiti kwenye mjadala wa mustakabali wake, bali anataka kuangalia namna ya kuboresha matokeo ya timu. “Kufikiria kuhusu muda wangu hapa hakunisaidii. Jambo muhimu ni viwango tunavyotaka kufikia na kutafuta suluhisho,” alisema baada ya kuanza msimu kwa changamoto.

Gharama za Kumfukuza Carrick Zaiweka Manchester United Kwenye PreshaKwa sasa, taarifa kutoka ndani ya klabu zinaonyesha hakuna mpango wa haraka wa kumfuta Carrick, huku uongozi ukitambua pia mazingira yaliyokuwepo katika usajili wa kikosi. United itaendelea kumtazama kocha huyo katika michezo ijayo, wakati presha kutoka kwa mashabiki na matokeo ya uwanjani ikiendelea kuwa sehemu ya mjadala kuhusu mustakabali wake.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.