Gordon Atua Barcelona Kwa Dau La Euro Milioni 80

Barcelona imethibitisha rasmi kumsajili winga wa England Anthony Gordon kutoka Newcastle United kwa mkataba wa miaka mitano katika usajili unaoripotiwa kugharimu euro milioni 80 (£69 milioni).

Gordon Atua Barcelona Kwa Dau La Euro Milioni 80Gordon amejiunga na miamba hiyo ya Hispania baada ya kuwa na mafanikio makubwa akiwa Newcastle tangu aliposajiliwa kutoka Everton mwaka 2023, akifunga mabao 39 na kutoa pasi 28 za mabao katika mechi 152 alizoichezea klabu hiyo.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Msimu uliopita, nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 aling’ara zaidi katika UEFA Champions League ambapo alifunga mabao 10 na kutoa pasi mbili za mabao, huku akisaidia Newcastle kufuzu michuano hiyo na kutwaa Kombe la EFL Cup.

Gordon Atua Barcelona Kwa Dau La Euro Milioni 80Akizungumza wakati wa utambulisho wake rasmi, Gordon aliwashangaza wengi kwa kuzungumza Kihispania kwa ufasaha na kueleza kuwa ndoto ya kuichezea Barcelona ilianza tangu utotoni.

Gordon Atua Barcelona Kwa Dau La Euro Milioni 80“Nimekuwa nikitamani kuichezea Barcelona tangu nikiwa mtoto. Nilijifunza Kihispania kwa sababu nilikuwa naamini siku moja nitafika hapa. Pia ninafurahia kucheza pamoja na Lamine Yamal na wachezaji wengine bora duniani,” alisema Gordon.

Gordon Atua Barcelona Kwa Dau La Euro Milioni 80Usajili huo unahitimisha uvumi wa muda mrefu kuhusu hatma yake kabla ya Kombe la Dunia, huku Barcelona ikiongeza nguvu katika kikosi chake kuelekea msimu mpya wa mashindano.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.