Antoine Griezmann amekiri hayupo katika ubora Barcelona na alisema alihitaji muda zaidi.

Griezmann amekuwa akipambana kuwa katika kiwango kizuri tangu atue Camp Nou kwa dau linaloripotiwa kufika€120m akitokea Atletico Madrid mwaka uliyopita.

Griezmann: Sipo Katika Ubora Wangu.
Antoine Griezmann

Mshambuliaji huyo amefunga magoli 17 katika michezo 58 katika mashindano yote ambao wapo nafasi ya 13 kwenye jedwali la LaLiga msimu 2020-21.

Griezmann amesmea alikuwa akijiandaa kukubali kukosolewa kutokana na kiwango chake lakini amesema imekuwa ni kipindi kigumu kwa klabu.

“Nimekubali yote sababu najua kwamba hatumuoni Griezmann bora,” aliiambia Movistar siku ya Jumatatu.

Aliongeza: “kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu tumekuwa na makocha watatu… hiyo siyo rahisi nahitaji muda wa kuzoeana na wachezaji wenzangu nawao pia kunizoea mimi lakini pia mabadiliko ya mfumo.

“Kwa kuongezea wagombea nafasi ya urais pia wanaongea kuhusu mimi, sidhani kama ni kitu kizuri kwangu mimi wao kuzungumza kuhusu mimi ilipaswa wazungumze hali au mimi siyo usajili mzuri.”

Griezmann amefunga magoli mawili na kutoa asisti moja katika michezo nane ya LaLiga msimu huu.

Lakini mazingira yake ya kiuchezaji yapo chini Barcelona ukiringanisha na Atletico Madrid, ni mara moja pekee ndani ya misimu mitano alikuwa na kiwango cha chini Atletico 2014-15.

Alitokea benchi mechi dhidi ya Atletico Madrid ambayo Barcelona alipoteza kwa 1-0, Barcelona itawatembelea Dynamo Kiev siku ya Jumanne katika Champions League.


USICHELEWE KUKAMATA MKWANJA HUU!

Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.

Meridianbet Tanzania Casino

SOMA ZAIDI

21 MAONI

  1. Griezman aliyokuwah nou camp kivuli tu antonio griezman amebaki atletico Madrid na france national team tunaye mjuwah sisi alikuwah kwny ubora wa Hali ya juu lakin co griezman wa sasa

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa