Guardiola Ampongeza Marmoush Katika Mbio za Ubingwa

Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola amesema mshambuliaji Omar Marmoush ana nafasi kubwa ya kuwa msaada muhimu katika michezo ya mwisho ya msimu huu wa England. City bado ina michezo minne muhimu ikiwemo fainali ya Kombe la FA huku ikisaka kumaliza msimu kwa mafanikio makubwa ya ndani.

Guardiola Ampongeza Marmoush Katika Mbio za UbingwaGuardiola amesema anahitaji kufanya mabadiliko ya kikosi ili kuhakikisha wachezaji wake wanabaki na nguvu kuelekea michezo iliyosalia pamoja na fainali ijayo. Kocha huyo alieleza kuwa baadhi ya wachezaji ambao hawajapata nafasi nyingi msimu huu wanapaswa kuwa tayari kusaidia timu inapohitajika.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

“Tumeshazungumza mara nyingi. Najua si rahisi kwao lakini nina uhakika katika michezo ijayo watapata nafasi ya kucheza,” alisema Guardiola. “Nataka kufanya mzunguko wa kikosi kwa sababu vinginevyo hatutakuwa tayari vya kutosha kuelekea fainali au mchezo dhidi ya Bournemouth.”

Guardiola Ampongeza Marmoush Katika Mbio za UbingwaGuardiola alimzungumzia kwa namna ya kipekee Marmoush ambaye alifunga bao akitokea benchi katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Brentford mwishoni mwa wiki. Kocha huyo alisema mshambuliaji huyo wa Misri ana uwezo mkubwa licha ya kukosa nafasi ya kucheza mara kwa mara kutokana na ushindani mkubwa ndani ya kikosi.

Guardiola Ampongeza Marmoush Katika Mbio za Ubingwa“Haswa Omar. Si rahisi kwa sababu kawaida unahitaji mshambuliaji mmoja tu. Yeye ni mshambuliaji halisi lakini Erling yupo,” alisema Guardiola akimzungumzia Erling Haaland ambaye amekuwa tegemeo kubwa la safu ya ushambuliaji ya City.

Guardiola Ampongeza Marmoush Katika Mbio za UbingwaGuardiola aliongeza kuwa licha ya Haaland kuwa muhimu sana kwa timu hiyo, mchango wa Marmoush katika dakika chache alizopewa umeonyesha ubora wake mkubwa. “Mchango wa Omar na idadi ya mabao aliyoifunga kwa dakika alizocheza ni mkubwa sana,” alisema kocha huyo wa Hispania.

Guardiola Ampongeza Marmoush Katika Mbio za UbingwaKwa upande mwingine, Guardiola pia alimpongeza Haaland baada ya kufikisha mabao 50 msimu huu akiwa na klabu na timu ya taifa ya Norway. “Ni jambo la ajabu, ingawa kulikuwa na kipindi mwezi Novemba alikuwa amechoka sana baada ya kurejea kutoka majukumu ya timu ya taifa. Ilikuwa kipindi kigumu kwake,” alisema Guardiola.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.