Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola amesema wachezaji wanapaswa kufanya vizuri zaidi uwanjani ili kuepuka malalamiko yanayohusiana na matumizi ya VAR, kuelekea mchezo wao dhidi ya Crystal Palace katika Ligi Kuu England.
Guardiola alikiri kuwa timu yake imewahi kuathiriwa na maamuzi ya VAR katika michezo mbalimbali iliyopita, hasa kwenye fainali za Kombe la FA za mwaka 2024 na 2025. Hata hivyo, alisisitiza kuwa suluhisho kubwa ni kwa timu kucheza vizuri zaidi badala ya kuwalaumu waamuzi.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
“Tulipoteza fainali mbili za FA Cup kwa sababu waamuzi hawakufanya kazi yao vizuri, hata VAR pia. Lakini hali kama hiyo ikitokea, maana yake sisi tunapaswa kufanya vizuri zaidi,” alisema Guardiola.
Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya VAR kuzua mjadala mwingine kufuatia West Ham United kunyimwa bao la kusawazisha dakika za mwisho dhidi ya Arsenal kwenye mchezo uliomalizika kwa ushindi wa mabao 1-0 kwa Arsenal. Ushindi huo uliifanya Arsenal kuendelea kuongoza ligi kwa tofauti ya pointi tano dhidi ya City.
Guardiola alisema tangu aanze kazi ya ukocha alijifunza kutegemea zaidi uwezo wa timu yake kuliko maamuzi ya waamuzi au VAR. “Siamini kitu chochote kirahisi tangu zamani. Kila mara nimejifunza kuwa unatakiwa kufanya vizuri zaidi kwa sababu VAR ni kama kurusha sarafu hewani, huwezi kujua matokeo yatakuwaje,” aliongeza.
Kocha huyo wa zamani wa FC Barcelona na Bayern Munich bado anaamini City walistahili kupata penalti mbili walipopoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya Manchester United katika fainali ya FA Cup miaka miwili iliyopita, kufuatia changamoto dhidi ya Erling Haaland kutoka kwa Lisandro Martínez na Kobbie Mainoo.
Licha ya hayo, Guardiola amesema kwa sasa akili yake ipo kwenye mchezo dhidi ya Crystal Palace, huku akiwataka wachezaji wake kubaki na umakini mkubwa katika mbio za ubingwa wa Premier League. “Kitu pekee tunachoweza kufanya ni kucheza vizuri zaidi. Ukipoteza umakini, unajiweka kwenye mazingira hatari. Sasa tunafikiria mchezo dhidi ya Crystal Palace pekee,” alisema Guardiola.


