Kwa muujibu Gazeti la Mirror la nchini United Kingdom limeripoti kuwa kocha mkuu wa Manchester City F.C., Pep Guardiola, amewaambia mabosi wa klabu hiyo kuwa ataondoka rasmi mwishoni mwa wiki hii baada ya kuitumikia timu hiyo kwa mafanikio makubwa.
Taarifa hiyo imeibua mjadala mkubwa miongoni mwa mashabiki wa soka duniani, huku Guardiola akihusishwa na mwisho wa enzi yake ndani ya klabu hiyo baada ya kushinda mataji mbalimbali ya ndani na kimataifa tangu alipowasili Etihad mwaka 2016.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, uongozi wa Manchester City tayari umeanza kufanya maandalizi ya kupata mrithi wa Guardiola, ambapo jina la Enzo Maresca limetajwa kuwa mbele katika nafasi hiyo.
Maresca ambaye aliwahi kuwa msaidizi wa Guardiola ndani ya Manchester City, pia amewahi kuzinoa Chelsea F.C. na Leicester City F.C., huku akitajwa kuwa mmoja wa makocha wanaoelewa vizuri falsafa ya Guardiola.
“Manchester City wanaamini Enzo Maresca ana uwezo wa kuendeleza mfumo na mafanikio yaliyojengwa na Pep Guardiola ndani ya klabu hiyo,” limeandika gazeti la Mirror.


