Guardiola Huenda Akaondoka Manchester City Mwisho wa Msimu

Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola anaripotiwa kuwa na uwezekano mkubwa wa kuondoka ndani ya klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu licha ya timu hiyo kuendelea kupambana kutwaa taji la Premier League.

Guardiola Huenda Akaondoka Manchester City Mwisho wa MsimuManchester City iliifunga Crystal Palace mabao 3-0 Jumatano usiku na kupunguza tofauti ya pointi dhidi ya vinara Arsenal hadi pointi mbili, huku City wakihitaji kushinda michezo yao miwili iliyosalia dhidi ya Bournemouth na Aston Villa ili kuendelea kuwa na matumaini ya ubingwa.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Hata hivyo, ripoti kutoka The Athletic zimeeleza kuwa kuna “uwezekano wa kweli” kwa Guardiola kuhitimisha safari yake ya miaka 10 ndani ya Etihad mwishoni mwa msimu huu, huku baadhi ya watu kutoka idara tofauti ndani ya kikosi cha kwanza wakiamini muda wake klabuni hapo umefika ukingoni.

Guardiola Huenda Akaondoka Manchester City Mwisho wa MsimuInaelezwa kuwa viongozi wa Manchester City tayari wameanza maandalizi ya maisha baada ya Guardiola, huku kocha wa Leicester City, Enzo Maresca akitajwa kuwa mmoja wa makocha wanaopewa nafasi kubwa ya kuchukua mikoba yake.

Guardiola Huenda Akaondoka Manchester City Mwisho wa Msimu“Tayari kuna hisia ndani ya klabu kuwa Guardiola anaweza kuondoka, na baadhi ya mipango ya baadaye imeanza kufanyiwa kazi,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo kuhusu hali ya sintofahamu iliyopo ndani ya City.

Guardiola Huenda Akaondoka Manchester City Mwisho wa MsimuTetesi hizo zimeongezeka zaidi baada ya kocha wa mazoezi ya viungo, Lorenzo Buenaventura, kuthibitisha kuwa ataondoka mwishoni mwa msimu huu baada ya kufanya kazi na Guardiola kwa zaidi ya miaka 15. Iwapo Guardiola ataamua kuondoka, Manchester City inatarajiwa kumpa heshima maalum katika mchezo wa mwisho wa nyumbani dhidi ya Aston Villa sambamba na wachezaji John Stones na Bernardo Silva wanaotarajiwa pia kuondoka klabuni hapo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.