Mshambuliaji nyota wa Norway, Erling Haaland, amesema timu yake ina nafasi ndogo sana ya kuifunga Brazil katika mchezo wa hatua ya 16 Bora ya michuano ya Dunia 2026 utakaochezwa mwishoni mwa wiki hii. Kauli hiyo imekuja baada ya Norway kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ivory Coast na kufuzu hatua inayofuata ya mashindano hayo.
Katika mchezo huo, Antonio Nusa aliitanguliza Norway kwa bao la kuvutia kipindi cha kwanza kabla ya Amad Diallo kuisawazishia Ivory Coast dakika 15 kabla ya mwisho wa mchezo. Hata hivyo, Haaland aliibuka shujaa kwa kufunga bao la ushindi katika dakika za mwisho na kuifikisha Norway hatua ya mtoano. Kwa sasa, Haaland ana mabao matano na ni miongoni mwa wafungaji vinara wa mashindano hayo.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Akizungumza kuhusu mchezo dhidi ya Brazil, Haaland hakuficha ukweli kuhusu ugumu wa kazi inayowasubiri. “Nafasi zetu ni ndogo sana,” alisema. Hata hivyo, aliongeza kuwa Norway haina cha kupoteza baada ya kuvuka matarajio ya wengi. “Hakuna aliyedhani tutafika hapa. Sasa tunakwenda kucheza dhidi ya Brazil, na hiyo ni changamoto kubwa na ya kipekee kwetu,” alisema mshambuliaji huyo wa Manchester City.
Haaland pia alionyesha hisia zake kuhusu mafanikio ya Norway kufika hatua hii ya mashindano. “Hii ni historia. Inahisi kama ndoto. Tumeweza kufuzu hatua ya mtoano kwa mara ya kwanza baada ya miaka 28 na sasa tunakwenda kukutana na Brazil. Kila kitu kuanzia hapa ni bonasi kwetu,” alisema kwa furaha kubwa baada ya mchezo.
Nahodha wa Norway, Martin Ødegaard, naye amesema kikosi hicho kina hamasa kubwa kuelekea pambano hilo. “Tumekua tukisikia simulizi za mechi kati ya Norway na Brazil kwa miaka mingi. Sasa sisi wenyewe tunapata nafasi ya kuandika historia yetu. Kwenye soka kila kitu kinawezekana, hivyo tunaamini tunaweza kufanya jambo kubwa tena,” alisema. Norway itamenyana na Brazil Jumapili katika Uwanja wa MetLife, New Jersey, huku mshindi wa mchezo huo akitinga robo fainali ya michuano ya Dunia 2026.


