Haaland Aitaka England Itwae Taji la Dunia Baada ya Kuiondoa Norway

Mshambuliaji wa Norway, Erling Haaland, amesema anatamani England ifike mbali na hatimaye kutwaa taji la Dunia 2026 baada ya timu yake kuondolewa kwa maumivu katika hatua ya robo fainali kufuatia kupoteza kwa mabao 3-1 dhidi ya England baada ya muda wa nyongeza mjini Miami.

Haaland Aitaka England Itwae Taji la Dunia Baada ya Kuiondoa NorwayNorway ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia Andreas Schjelderup kipindi cha kwanza, lakini England ilirejea kwa nguvu huku Jude Bellingham akifunga mabao mawili yaliyoiongoza timu hiyo kutinga nusu fainali na kuhitimisha safari ya kihistoria ya Norway katika michuano ya Dunia, ikiwa ni mara yao ya kwanza kushiriki mashindano hayo baada ya miaka 28.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Akizungumza baada ya mchezo huo, Haaland alisema ana sababu binafsi ya kuitakia mema England kutokana na historia yake ya kuzaliwa nchini humo na pia uwepo wa baadhi ya wachezaji wenzake wa Manchester City ndani ya kikosi hicho. Nyota huyo alizaliwa mjini Leeds wakati baba yake, Alf-Inge Haaland, akiichezea Leeds United.

Haaland Aitaka England Itwae Taji la Dunia Baada ya Kuiondoa Norway“Kwa nini nisiiunge mkono England? Nina wachezaji wenzangu wengi wa Manchester City kwenye kikosi hicho. Nimekuwa nikiifuatilia England tangu nikiwa mtoto, hata nilikuwa na jezi ya England kabla sijawa na ya Norway. Ni nchi nzuri na ninawatakia kila la heri,” amesema Haaland.

Haaland Aitaka England Itwae Taji la Dunia Baada ya Kuiondoa NorwayLicha ya kuaga mashindano, Haaland ameondoka akiwa mmoja wa nyota bora wamichuano ya Dunia baada ya kufunga mabao saba, rekodi iliyomfanya kuingia kwenye kinyang’anyiro cha Kiatu cha Dhahabu pamoja na Harry Kane, Kylian Mbappe na Lionel Messi. “Tulionyesha kuwa Norway inaweza kuwa miongoni mwa mataifa makubwa ya soka duniani. Tulipambana vizuri dhidi ya England na ninajivunia kila tulichokifanya tangu tulipofuzu hadi tulipofika hapa Marekani,” amesema mshambuliaji huyo.

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.