Haaland Atupia Mawili, Norway Yafuzu Hatua ya 32 Bora

Mshambuliaji nyota Erling Haaland alifunga mabao mawili na kuiongoza Norway kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Senegal, matokeo yaliyoihakikishia nafasi ya kutinga hatua ya 32 bora ya mashindano ya Dunia 2026.

Haaland Atupia Mawili, Norway Yafuzu Hatua ya 32 BoraBaada ya kuifunga Iraq mabao 4-1 katika mchezo wao wa kwanza, Norway ilihitaji ushindi mwingine ili kuthibitisha kufuzu kwake. Kikosi hicho kilianza mchezo kwa kasi kubwa na kutengeneza nafasi kadhaa za mabao, huku golikipa wa Senegal, Edouard Mendy, akifanya kazi ya ziada kuokoa hatari zilizokuwa zikielekezwa langoni mwake.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Dakika chache kabla ya mapumziko ya kipindi cha kwanza, Norway ilipata bao la kuongoza baada ya beki Kalidou Koulibaly kufanya makosa ya kupoteza mpira karibu na eneo la hatari. Marcus Holmgren Pedersen alitumia vizuri kosa hilo na kuifungia Norway bao la kwanza. “Tulijua ushindi ungekuwa muhimu sana kwetu, hivyo tulipambana kwa nguvu tangu mwanzo wa mchezo,” ilielezwa kutoka kambi ya Norway baada ya mechi.

Haaland Atupia Mawili, Norway Yafuzu Hatua ya 32 BoraKipindi cha pili kilianza kwa Haaland kuonyesha ubora wake alipofunga bao la pili kufuatia shambulizi la kushtukiza lililoanzishwa na nahodha Martin Odegaard. Senegal walijibu haraka kupitia Ismaila Sarr, lakini Haaland aliifungia Norway bao la tatu dakika chache baadaye na kufikisha mabao manne kwenye mashindano hayo, akibaki nyuma ya Lionel Messi katika mbio za kuwania Kiatu cha Dhahabu.

Haaland Atupia Mawili, Norway Yafuzu Hatua ya 32 BoraLicha ya Sarr kufunga bao lake la pili katika dakika za nyongeza, Senegal walishindwa kurejea mchezoni. Ushindi huo unaifanya Norway kufuzu rasmi hatua ya mtoano na sasa itakutana na Ufaransa katika mchezo wa mwisho wa Kundi I kuamua mshindi wa kundi hilo, huku Senegal ikibakiwa na matumaini ya mwisho ya kufuzu kupitia nafasi ya timu bora za tatu iwapo itaifunga Iraq.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.