Hatma ya Rashford Yatia Mashaka Barca, PSG na AC Milan Zaanza Kumnyemelea

Mustakabali wa nyota wa England, Marcus Rashford, umeanza kuwa shakani huku hali ya kifedha ya FC Barcelona ikizua sintofahamu kuhusu hatma yake ya kudumu katika klabu hiyo ya Hispania.

Hatma ya Rashford Yatia Mashaka Barca, PSG na AC Milan Zaanza KumnyemeleaRashford, ambaye yupo kwa mkopo akitokea Manchester United, amekuwa katika kiwango bora na kuvutia mashabiki wa Camp Nou, hali iliyowafanya wengi kutarajia aendelee kusalia kwa mkataba wa kudumu.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa  

Hata hivyo, taarifa zinaeleza kuwa Barcelona inasuasua kutumia kipengele cha kumnunua kwa Pauni milioni 26 (€30M) kutokana na changamoto za kifedha zinazoikumba klabu hiyo kwa sasa.

Hatma ya Rashford Yatia Mashaka Barca, PSG na AC Milan Zaanza KumnyemeleaKwa upande wa Manchester United, uongozi wa klabu hiyo umesisitiza msimamo wao kwa kukataa maombi ya kupunguziwa bei au kuongeza muda wa mkopo, ukitaka malipo kamili yafanywe mara moja. Chanzo kimoja kilinukuliwa kikisema, “Tunataka thamani kamili ya mchezaji wetu, hakuna mazungumzo ya punguzo kwa sasa.”

Wakati sintofahamu hiyo ikiendelea, vigogo wa Ulaya wakiwemo Paris Saint-Germain na AC Milan wameanza kufuatilia kwa karibu maendeleo ya dili hilo, wakijiandaa kuwasilisha ofa endapo Barcelona itashindwa kukamilisha usajili huo.

Hatma ya Rashford Yatia Mashaka Barca, PSG na AC Milan Zaanza KumnyemeleaIngawa Rashford mwenyewe anatamani kubaki Camp Nou, ripoti zinaeleza kuwa uamuzi wa mwisho utategemea uwezo wa kifedha wa Barcelona, huku mkataba wake na Manchester United ukiendelea hadi mwaka 2028, jambo linaloipa klabu hiyo nguvu ya kufanya maamuzi ya mwisho.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.