KLABU ya Yanga imeandika historia nyingine jana Ijumaa, Agosti 19, 2022 baada ya kuingia makubaliano na kusaini mkataba wa miaka miwili wa kufanya kazi na kampuni iliyobobea katika masoko ambayo ni ya wazawa iitwayo Jackson Group.
Mhandisi Hersi Said
Mhandisi Hersi Said
Akizungumza kabla ya kusaini mkataba huo, Rais wa Klabu ya Yanga, Mhandisi Hersi Said amesema baada ya kufanya mabadiliko ya Katiba na kuruhusu umiliki wa hisa asilimia 51 kwa Wanachama na asilimia 49 kwa wawekezaji, klabu hiyo sasa imefungua milango kwa wawekezaji kuja kuwekeza na kufanya biashara na Yanga.

“Kabla ya kuingia madarakani, moja ya ajenda yangu na moja ya mambo ambayo niliahidi wakati wa kampeni ni kuifanya Yanga iwe kibiashara ili iingize pesa.

“Yanga ndiyo klabu kongwe hapa Tanzania na ndiyo klabu yenye mataji mengi na wanachama wengi, lakini ukubwa na thamani yake hauendani.

Mhandisi Hersi Said
Mhandisi Hersi Said

“Hivyo tumeona badala ya kuajiri Mkurugenzi wa Masoko tukamlipa pesa, ni bora kutafuta kampuni ambayo ina uzoefu mkubwa kwenye masuala ya masoko.

“Ili watuletee wawekezaji na kutushauri mbinu bora za klabu kufanya biashara na kuingiza pesa, klabu itaingiza pesa na itakuwa rahisi hata kujenga uwanja kama nilivyoahidi.

“Hatutaweza kujenga uwanja ama kupata maendeleo makubwa kama klabu hatuna mipango endelevu ya kiuchumi na yenye tija. Hivyo tunawakaribisha wawekezaji na wafanyabiashara kuja kuwekeza Yanga,” amesema Hersi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kampuni ya Jackson Group, Kelvin Twisa amesema wameamua kuingia makubaliano hayo na Yanga baada ya kuona kwamba ndiyo klabu bora Tanzania na yenye uongozi unaojielewa, wataweza kusimamia vyema haki za mdhamini.

 

Kwa taarifa za kimichezo na uchambuzi sasa unaweza kutazama video hizo kwa kupitia youtube . USISAHAU KU SUBSCRIBE


 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa