“Hili Ni Zaidi ya Ushindi” – Scaloni Aeleza Fahari Yake kwa Wachezaji wa Argentina

Kocha wa timu ya taifa ya Argentina, Lionel Scaloni, ameshindwa kuficha hisia zake baada ya timu yake kufanya mabadiliko makubwa na kuifunga England mabao 2-1 katika nusu fainali ya michuano ya Dunia, ushindi uliowapeleka kwenye fainali ya michuano hiyo kwa mara ya pili chini ya uongozi wake.

“Hili Ni Zaidi ya Ushindi” – Scaloni Aeleza Fahari Yake kwa Wachezaji wa ArgentinaArgentina ilikumbana na wakati mgumu baada ya kufungwa bao la kwanza na England katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Mercedes-Benz Stadium. Hata hivyo, kikosi hicho kilionyesha moyo wa kupambana na kubadilisha matokeo, jambo lililomfanya Scaloni kupongeza wachezaji wake kwa kujitoa kwao ndani ya uwanja.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

“Nawaambia watu wafurahie hili. Ni jambo la ajabu. Wafurahie kufuzu kwa fainali na waone jinsi ilivyo muhimu kuwa hapa. Waishukuru timu hii ya wachezaji, kwa sababu ni vigumu kuelezea kundi hili kwa maneno. Kwa kweli sauti yangu inatetemeka kwa sababu hili linaonyesha mambo mengi, lilikuwa jambo la kugusa moyo,” alisema Scaloni baada ya mchezo.

“Hili Ni Zaidi ya Ushindi” – Scaloni Aeleza Fahari Yake kwa Wachezaji wa ArgentinaKocha huyo wa Argentina alisisitiza kuwa mafanikio hayo hayajatokana na mbinu pekee au maandalizi ya kimwili, bali yamejengwa kutokana na umoja, tabia na moyo wa kupigana wa wachezaji wake ambao ameuita kuwa ni wa kipekee katika soka la kisasa. “Baada ya kufungwa bao, tuliweza kutengeneza nafasi nyingi za kufunga. Unafurahia kwa sababu timu ilionyesha kuwa inapambana hadi mwisho, na kwangu hilo ndilo jambo la msingi zaidi,” alisema Scaloni.

“Hili Ni Zaidi ya Ushindi” – Scaloni Aeleza Fahari Yake kwa Wachezaji wa ArgentinaScaloni alieleza kuwa hata kama Argentina ingeshindwa, bado angejivunia namna wachezaji wake walivyocheza na kutoa kila walichokuwa nacho uwanjani. Kwa mujibu wake, mwitikio wa timu baada ya kufungwa bao ulikuwa mfano wa kile anachotamani kuona katika mchezo wa soka. “Tungeondoka tukiwa na huzuni, lakini tukijua kuwa tumetoa kila kitu uwanjani na kucheza mchezo tuliopaswa kucheza. Baada ya bao lao, ilikuwa ni ushahidi wa kila kitu tunachotaka kuona kwenye soka,” aliongeza.

“Hili Ni Zaidi ya Ushindi” – Scaloni Aeleza Fahari Yake kwa Wachezaji wa ArgentinaKocha huyo amesema kutwaa ubingwa wa dunia si kitu pekee kinachomsukuma, bali namna timu yake inavyokabiliana na changamoto ndiyo jambo muhimu zaidi kwake.  “Sio ushindi pekee ndio unanipa motisha. Ningependa kuwa bingwa wa dunia, nani asingependa? Lakini hilo sio linalonisukuma. Kitu muhimu zaidi ni namna tunavyokabiliana na hali mbalimbali. Jinsi tulivyorejea mwishoni mwa mchezo ni mfano wa ajabu,” alisema Scaloni.

“Hili Ni Zaidi ya Ushindi” – Scaloni Aeleza Fahari Yake kwa Wachezaji wa ArgentinaArgentina sasa itachuana na Hispania katika fainali ya michuano ya Dunia itakayochezwa Jumapili kwenye uwanja wa MetLife Stadium, New York/New Jersey. Mchezo huo utakuwa fainali ya kwanza ya michuano ya Dunia kukutanisha bingwa wa Ulaya dhidi ya bingwa wa Copa América.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.