Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Misri, Hossam Hassan, amesema hatatazama tena mechi zozote za michuano ya Dunia 2026 baada ya timu yake kuondolewa kwa maumivu na mabingwa watetezi Argentina katika hatua ya 16 bora. Misri ilikuwa mbele kwa mabao 2-0 hadi dakika ya 79 kabla ya Argentina kufanya comeback ya kushangaza na kushinda kwa mabao 3-2.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Bao la Mostafa Zico lililofungwa dakika ya 62 lilibatilishwa baada ya ukaguzi wa VAR kubaini kuwa kulikuwa na madhambi katika maandalizi ya bao hilo. Aidha, Misri ilidai ilinyimwa penalti kufuatia Hamdy Fathy kuvutwa ndani ya eneo la hatari, kabla ya Argentina kufunga bao la ushindi dakika ya 92 na kuzima ndoto za Wamisri kufuzu robo fainali.
Hassan alisisitiza kuwa, licha ya makosa yaliyofanywa na wachezaji wake, kilichoumiza zaidi ni maamuzi ya waamuzi. “Ninachukia kupoteza, lakini kinachoniumiza zaidi ni kupoteza kwa namna isiyo ya haki. Mashabiki wasihuzunike, tulifanya kila tuwezalo kuwapa furaha. Kilichonifurahisha ni kwamba wachezaji wangu walifuata mpango wa mchezo na walipambana kwa kiwango cha juu,” alisema.
Kocha huyo aliwapongeza wachezaji wake kwa ushindani waliouonyesha dhidi ya Argentina, akibainisha kuwa wengi wao wanacheza ligi ya ndani ya Misri tofauti na mataifa mengi yenye wachezaji wanaocheza Ulaya. “Nimeridhishwa sana na juhudi zao. Isipokuwa Mohamed Salah na Omar Marmoush, wengi wa wachezaji wetu wanatoka ligi ya ndani, lakini bado tuliweza kushindana na timu yoyote duniani,” alihitimisha Hassan.


