Kama Hulk atarejea katika klabu ya Porto, basi kocha Andrea Villas na mashabiki wa Porto watajivunia.

Mshambuliaji huyo wa Brazil ameonekana kutaka kurejea katika dimba la Estadio do Dragao mwaka 2021 baada ya kusema kupitia mitandao ya kijamii kuwa hato ongeza mkataba mpya na Shanghai SIPG.

Huenda Hulk Akarejea Porto, Furaha kwa Villas-Boas.
Hulk

Hulk ameshinda mataji 11 akiwa Porto ikuhisha mataji manne ya ligi na Europa League mwaka 2010-2011, kabla hajatimkia Zenit mwaka 2012 kwa du la €60m.

Alihamia katika ligi ya Chinese Super Laegue miaka minne baadaye na kufanikiwa kushinda taji la ndani na FA Super Cup.

Hulk alicheza chini ya mwalimu Villas-Boas akiwa Porto, Zenit na Shanghai SIPG na kocha mpya wa sasa wa Marseille amekiri kuwa itakuwa jambo kubwa la kusherehekea kama mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 atareja Ureno.

“Nimefanya naye kazi katika vilabu vitatu tofauti,” alisema. “Nataka Hulk achague kwa uhuru wake.

“Kama akichagua Porto na Poto wanataka hilo na inawezekana ikawa klabu yake ya mwisho katika soka lake, pia ni jambo ambalo litatufanya sisi mashabiki wa Porto tujivunie.

Bosi wa Marseille Villas-Boas atawakabili Porto katika Champions League siku ya Jumatano huku akiwa anajua ushindi ni kitu kinacho hitajika ilikupata nafasi ya kusonga katika 16 bora.

Timu hiyo ya Ligue 1 inashika mkia katika kundi C baada ya kupoteza michezo mitatu ya ufunguzi kwa Manchester City, Olympiacos na Porto wakati pia ndiyo timu pekee msimu huu kutofunga goli lolote kwenye mashindano hayo.


USICHELEWE KUKAMATA MKWANJA HUU!

Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.

Meridianbet Tanzania Casino

SOMA ZAIDI

22 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa