Hugo Broos athibitisha kuondoka Rasmi Afrika Kusini Bafana Bafana

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Afrika Kusini, Hugo Broos, amethibitisha rasmi kuwa hataendelea kuinoa Bafana Bafana, akimaliza uvumi uliodumu kwa takribani wiki mbili kuhusu hatma yake baada ya michuano ya Dunia 2026. Broos mwenye umri wa miaka 74 amesema uamuzi wake wa kustaafu ukocha hauwezi kubadilika licha ya kuwahi kuonyesha uwezekano wa kubaki baada ya Afrika Kusini kutolewa na wenyeji Canada katika hatua ya 32 bora Juni 28.

Hugo Broos athibitisha kuondoka Rasmi Afrika Kusini Bafana BafanaAkizungumza nchini kwao Ubelgiji, Broos alisema amefanya mazungumzo na uongozi wa Shirikisho la Soka Afrika Kusini (SAFA), ambao umemueleza kuwa ungependa aendelee kulitumikia taifa hilo katika nafasi tofauti kama mshauri au mtaalamu wa utafutaji wa vipaji. “Sitaendelea kuwa kocha tena, huo ni uamuzi wa mwisho. Kama watanihitaji katika nafasi nyingine kama ushauri au scouting, hilo linawezekana, lakini sitaki tena maisha ya soka yawe sehemu ya kila saa ya maisha yangu,” alisema Broos.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Kocha huyo aliongeza kuwa atarejea Afrika Kusini mwishoni mwa mwezi Julai kwa ajili ya kuaga rasmi na kusikiliza pendekezo la SAFA kuhusu nafasi mpya. Pia alitania kuhusu maisha yake ya baada ya ukocha akisema, “Mke wangu anafurahia kuona ninaacha ukocha, lakini tayari ameniambia nihakikishe simsumbui nyumbani. Kama nitakuwa nikisafiri Afrika Kusini kwa wiki chache kila baada ya miezi miwili, hilo ni bora kuliko kukaa nyumbani bila shughuli.”

Hugo Broos athibitisha kuondoka Rasmi Afrika Kusini Bafana BafanaBroos aliteuliwa kuinoa Afrika Kusini mwezi Mei 2021 na kuwa kocha aliyedumu kwa muda mrefu zaidi katika historia ya timu hiyo. Chini ya uongozi wake, Bafana Bafana ilifuzu michuano ya Dunia kwa mara ya kwanza baada ya miaka 16, ikafuzu pia mara mbili mfululizo fainali za Kombe la Mataifa Afrika (AFCON) na kutwaa medali ya shaba katika michuano ya mwaka 2023, huku akijijengea heshima kubwa kutoka kwa wachezaji na mashabiki.

Hugo Broos athibitisha kuondoka Rasmi Afrika Kusini Bafana BafanaBaada ya kuthibitishwa kuondoka kwake, macho sasa yanaelekezwa kwa kocha atakayechukua mikoba yake, ambapo Pitso Mosimane anatajwa kuwa mgombea anayepewa nafasi kubwa kurejea kuinoa timu hiyo kwa mara ya tatu. Mosimane aliwahi kuiongoza Afrika Kusini katika michezo 23, akishinda mechi tisa, kutoka sare mara 10 na kupoteza nne pekee, huku timu yake ikifunga mabao 17 na kuruhusu mabao nane tu.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.