Tottenham wanaweza kumkosa mlinda mlango wao Hugo Lloris, kwenye mechi ya dabi ya London kaskazini huko Arsenal mnamo Oktoba.

Kipa huyo mwenye umri wa miaka 35 aling’ara sana wakati Spurs iliposhinda 6-2 dhidi ya Leicester wikendi iliyopita, huku akizuia mpira wa kichwa uliopigwa na Patson Daka kipindi cha pili na kuwazuia Foxes kufanya matokeo kuwa 3-3.

 

Hugo Lloris Kuwakosa Arsenal.

Lloris alijiunga na timu ya taifa ya Ufaransa siku ya Jumatatu kabla ya mechi za wiki hii za Ligi ya Mataifa kati ya Austria na Denmark lakini ameondoka kambini huko Clairefontaine.

Amegundulika kuwa na jeraha kwenye paja lake la mguu wa kulia, ambalo litamhusu kocha wa Spurs Antonio Conte kutafuta mbadala wake kwenye safari ya kwenda Arsenal mwezi Oktoba 1.

“Alipowasili Jumatatu asubuhi katika Kituo cha Kitaifa cha Soka huko Clairefontaine, Hugo Lloris aliwasiliana na Dk Franck Le Gall,” taarifa kutoka Shirikisho la Soka la Ufaransa iliandika.

“Jeraha dogo la paja la mguu wa kulia limegunduliwa kwa kipa wa Tottenham.

“Kwa hivyo hayupo kwenye mechi mbili dhidi ya Austria siku ya Alhamisi huko Stade de France na Denmark siku ya Jumapili.”

 

Hugo Lloris Kuwakosa Arsenal.

Lloris ni mchezaji wa pili wa Tottenham kujiondoa kwenye majukumu ya kimataifa baada ya Ben Davies, kulazimika kujiondoa kwenye kikosi cha Wales kufuatia jeraha la goti lake. Pia anakabiliwa na kinyang’anyiro dhidi ya muda ili kuwa fiti kumenyana na Arsenal.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa