Majira ya joto kwenye LaLiga ni maalum kabisa kwa usajili wa wachezaji. Ni wakati ambao vilabu hujiimarisha na kufanya marekebisho yanayohitajika kwenye vikosi vyao kabla ya msimu mpya na ni kipindi cha msisimko na matumaini mapya kwa mashabiki.

Kuna sheria ya udhibiti ipo sheria hiyo ndiyo inayoisummbua Barcelona mpaka hii leo juu ya ya matumizi ya pesa, Lakini mchakato huu unafanyaje kazi kutoka nyuma ya pazia? Je, klabu inapaswa kufanya nini inaposajili mchezaji ili acheze LaLiga? Je, ni nini kinahusika katika sheria za Udhibiti wa Uchumi na Ukomo wa Gharama za Kikosi ambazo zimeidhinishwa kwenye LaLiga? Ripoti hii maalum inatupa jicho jinsi ambavyo usajili ndani ya LaLiga unavyokuwa.

LALIGA, Ifahamu Kanuni ya LaLiga Ya Kikomo cha Gharama za Kikosi unavyofanya kazi, Meridianbet

Udhibiti wa Kiuchumi ni mfumo wa udhibiti ambao uliwekwa na vilabu vya LaLiga na SADs (kampuni za umma zilizo na mipaka), iliyozinduliwa mnamo 2013 kwa madhumuni ya wazi ya kuhakikisha uendelevu wa mashindano na vilabu vyenyewe kupitia ukaguzi wa kifedha.

Mfumo huu unatumika kwenye timu za ligi kuu, ambayo ni LaLiga Santander, na katika ligi ya daraja LaLiga SmartBank pia, kwa hivyo vilabu vyote vinavyoshiriki lazima zizingatie sheria sawa. Udhibiti wa Kiuchumi wa LaLiga ni wa kuzuia na unakaa pamoja na hatua za rejea Haki ya usawa wa Kifedha wa UEFA.

LALIGA, Ifahamu Kanuni ya LaLiga Ya Kikomo cha Gharama za Kikosi unavyofanya kazi, Meridianbet

Vilabu vinajua ni kiasi gani wanaweza kutumia mapema, na kufanya iwe rahisi kukaa ndani ya mipaka na kuzuia ongezeko la deni. Ukiangalia ligi kuu tano za Ulaya, kipimo hiki kinatofautisha LaLiga na nyingine linapokuja suala la soko la uhamisho.

Wakati wa kufanya usajili, moja ya nguzo za Udhibiti wa Uchumi ni ile ya Kikomo cha Gharama za Kikosi (SCL). Hii ni, kwa maneno mengine, kiasi ambacho kila klabu inaweza kutumia kwenye kikosi chao. Ikumbukwe kikosi hicho kinaundwa na sehemu zinazoweza kusajiliwa na zisizosajiliwa. Kikosi cha Usajili kinahusu wachezaji 25, kocha mkuu, kocha msaidizi, kocha wa mazoezi ya viungo na makocha wengine wenye majukumu yanayofanana.

LALIGA, Ifahamu Kanuni ya LaLiga Ya Kikomo cha Gharama za Kikosi unavyofanya kazi, Meridianbet

Mfumo huu hauhusu tu mishahara ya wataalamu hawa, lakini na mambo mengine mbalimbali pia, kama vile malipo ya kuvunja mkataba, malipo ya haki za picha, ada za wakala, malipo ya haki za uhamisho, gharama za mikopo, michango ya hifadhi ya jamii, fidia, 25% ya bei ya usajili (wakati kuna uwezekano mkubwa wa kutekelezwa), ada za leseni na malipo mengine. Kwa hivyo, mchezaji yeyote mpya klabu anayesajiliwa lazima awe ndani ya SCL ya klabu.

Kanuni hii imeleta faida gani kwenye vilabu.

Kanuni hii tayari imetoa faida kuanzia 2014/15 hadi 2019/20, usawa wa vilabu uliongezeka kwa 250%. Wakati huo huo, deni linalodaiwa na mashirika ya umma limepungua kutoka paundi €650m mwaka wa 2013 hadi paundi €17m pekee mwaka 2021. pia malalamiko kutoka kwa wachezaji kuhusu kutolipwa yamepungua sana, kutoka thamani ya paundi €89m mwaka wa 2011 hadi paundi €1.5m mwaka wa 2021.

Kwa muda tangu kuanzishwa kwa Udhibiti wa Kiuchumi, matokeo chanya ya nje ya uwanja yameambatana na mafanikio ndani ya uwanja, kwani mataji 17 kati ya 26 ya Europa yaliyopita wakati huu yamechukuliwa na timu za Hispania.

Ripoti hii itaendelea…………. #Itsallabout #LaligaSantader

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa