Naoya Inoue bondia wa Japan ambaye shughuli yake ulingoni si ndogo amechapa kwa KO katika raundi ya pili bondia mtata Nonito Donaire kwenye ukumbi wa Saitama Super Arena siku ya Jumanne Juni 7.
Baada ya kumdondoshea konde la mkono wa kulia mwishoni mwa raundi ya kwanza kengele ilimsaidia Donaire ambaye alidondoka nakuanza kuhesabiwa na mwamuzi lakini raundi pili Inoue aliendeleza alipoishia na mwamuzi alilazimika kumaliza pambano zikiwa zimesalia dakika 1 na 38 kutimiza raundi ya pili.
Inoue ambaye ana umri wa miaka 29 ameboresha rekodi yake ya kupigana mapambano 23 na kushinda yote huku 20 akishinda kwa KO hili lilikuwa ni pambano lake la pili dhidi ya Donaire ambaye ana muri wa miaka 39 ambapo katia pambano la kwanza Inoue alishinda kwa pointi kwenye pambano la raundi 12.
Naoya amemchapa Donaire kikatili na kuongeza taji la uzani wa bantam WBC kwenye mataji yake ya WBA na IBF.
“Nilipokea konde m oja zito katika raundi ya kwanza konde ambalo liliniamsha” Alisema Inoue baada ya pambano.
“Nilijua napaswa kushinda pambano hili kwa hiyo nilijaribu kulimaliza mapema kwenye raundi ya pili.
SHINDA SAMSUNG A32 NA AVIATOR
SHINDA Samsung A32 ukiwa na mchezo wa Aviator kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet! Kwea pipa ukusanye zawadi zako pamoja na ushindi mnono wa mkwanja!
SOMA ZAIDI HAPA