KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Stephane Aziz KI baada ya timu yake kutolewa kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Mamelodi Sundowns kwa mikwaju ya penati hatua ya robo fainali, ameandika katika ukurasa wake wa Instagram ujumbe wa kuwashukuru mashabiki kwa kuwa nao pamoja kwenye safari ya michuano hiyo msimu huu 2023/2024. Odds kubwa, kasino ya mtandaoni na michezo ya sloti ni njia rahisi ya kukupa mtonyo mrefu. Ingia mchezoni hapa.
Aziz KI ameandika.
“Tumeonyesha sisi ni timu kubwa na tuna malengo, licha ya changamoto zote tutafika tunapotaka kwenda, kwani sisi ni timu kubwa, haikuwezekana msimu huu lakini tutakuwa bora zaidi wakati mwingine.”
“Kipekee kabisa niwashukuru wote waliokuwa na sisi kwenye safari hii hasa Rais wa nchi, Mama Samia Suluhu Hassan kwa kujitolea kwake kwetu ili tuweze kuwa bora zaidi katika mechi zetu, tulienda Afrika Kusini kama washindi na tutarudi Tanzania washindi pia, ila tumejifunza mengi ya kutufanya kuwa bora zaidi wakati mwingie.”
Katika ujumbe huo Aziz KI pia amemjibu shabiki aliyeandika kuhusu yeye kuondoka klabuni hapo msimu ujao kutokana na kufanya vizuri kwenye mashindano na klabu nyingi kutaka huduma yake.
Ameandika; “Huna baya mwamba sana, najua msimu ujao utaondoka maana naona Mamelodi wanataka kukusajili, najua utaondoka.”
KI amejibu; “Sina matarajio ya kuondoka Yanga kwa sasa kwani sijafanikisha malengo yaliyonileta hapa, bado klabu hii ninayoipenda kwa moyo wangu wote inanidai, hata pesa haitaweza kujaza upendo nilionao kwa klabu hii, lala kwa amani shabiki bado sijamaliza dhamira yangu.”
Ikumbukwe Aziz KI amebakiza miezi minne kumaliza mkataba wake na Yanga ambao alisaini msimu wa 2022\2023. Jisajili na Meridianbet upate bonasi za kasino kibao na odds kubwa za ubashiri kwa machaguo kibao.