Kesi ya Mohamed Salah inazidi kuvutia dunia ya soka huku klabu ya Inter Miami CF ikiripotiwa kujiandaa kuwasilisha ofa rasmi ya kumsajili mshambuliaji huyo wa Liverpool.
Kwa mujibu wa ripoti ya The Independent, Inter Miami inatarajia kumuunganisha Salah na nyota Lionel Messi na Luis Suarez kuunda safu ya ushambuliaji yenye hofu kubwa zaidi duniani.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Hata hivyo, ili kufanya nafasi ya mshahara wa Salah, Inter Miami itabidi kumuondoa mmoja wa wachezaji wake wa daraja la juu, ambao kwa sasa ni Messi, Rodrigo De Paul, na German Berterame. Hii inatokea baada ya Salah kutangaza kuondoka Anfield mwishoni mwa msimu huu, jambo lililozua shauku kwa klabu kubwa za Saudi Arabia na sasa Marekani.
Hata hivyo, ushindani wa kumsajili Salah umekua mkali kutokana na klabu ya Al-Ittihad FC, ambayo imefufua nia yake ya kumsajili mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Misri. Itakumbukwa kuwa mwaka 2023, Liverpool iliikataa ofa ya pauni milioni 150 kutoka Al-Ittihad, lakini sasa hali imebadilika.
Salah, mwenye umri wa miaka 33, atakuwa mchezaji huru baada ya mkataba wake na Liverpool kumalizika mwishoni mwa msimu huu, na kufanya safu ya uhamisho wake kuwa kati ya za kuvutia zaidi kwenye soka la kimataifa mwaka huu.

