Klabu ya Inter Milan ya nchini Italia imekumbana na kipigo chao cha tatu msimu huu katika ligi kuu nchini Italia baada ya kufungwa na klabu ya Udinese mapema mchana wa leo.

Klabu hiyo iliokua katika dimba la Dacia Arena dhidi ya wenyeji Udinese ambao waliwatembezea kicha cha mabao matatu kwa moja na kuwafanya vijana hao wa Simeone Inzaghi kushinsa michezo minne tu kati ya saba waliyoingia uwanjani msimu huu.

inter milanInter milan walikua wa kwanza kupata bao mapema kabisa kupitia kiungo wa raia wa Italia Nicolo Barrela dakika ya tano ya mchezo kabla ya Milan skriniar kujifunga mnao dakika ya 22 ya mchezo na kufanya mchezo uwe bao moja kwa moja mpaka kipindi cha kwanza kinakamilika huku Udinise ikiwa inaonekana kuumilikim mchezo zaidi.

Kipindi cha pili mambo yaliendelea kua magumu kwa vijana wa Inzaghi japo walikua wanaongoza kwa umiliki wa mpira mpaka pale dakika ya 85 ya mchezo mchezaji Bijol kuweka kambani bao la pili na kuwafanya Udinese kuomgoza mchezo kabla ya Arslan kuongeza bao la tatu katika dakika za nyomgeza na kufanya mchezo kumalizika kwa mabao matatu kwa moja.

Mabingwa hao wa misimu miwili nyuma mpaka sasa wamevuna alama 12 pekee na wakiwa nafasi ya sita ya msimamo huku Udinese wao wakikwea kileleni mwa msimamo na alama zao kumi na saba.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa