Inter Milan na Arturo Vidal wamefikia makubaliano ya kuvunja mkataba na klabu ya hiyo mchezaji huyo wa Chile anakaribia kujiunga na klabu ya Flamengo.

Kwa mujibu wa taarifa ni kwamba Inter wanapaswa kumlipa Vidal kiasi cha euro milioni 4 kusitisha mkataba wao baada ya kuitumikia miaka miwili mkataba wa awali ulikuwa uanisha mwaka 2022 lakini kulikuwa na kipengele cha kumuongeza mwaka mmoja.

Msimu uliyopita Vidal alianza katika michezo miwili ya Serie A na klabu hiyo ya Serie A ilikuwa na mpango wa kumuachia.

Siku ya Juamtatu  Inter walithibitisha kwamba wamefikia maridhiano ya pande zote  kusitisha mkataba wa Vidal.

Wiki iliyopita Vidal alionekana akiwa Rio de Janeiro akiwa kwenye picha na mashabiki wa Flamengo na inasemekana yupo mbioni kujiiungana klabu hiyo ya Serie A ya Brazil.

Vidal alijiunga na Bayer Leverkusen mwaka 2007 kabla ya kutimikia Juventus na mwaka 2015 akajiunga tena na Bundesliga akiwa na Bayern Munich na Baadaye alijunga  na Barcelona ambako alitumia miaka miwili na kurejea Italia.


CHEZA KASINO HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa