Inter Milan imeonyesha kurejea katika ubora wake baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Feyenoord katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya uliopigwa kwenye Uwanja wa De Kuip, matokeo yaliyowasaidia kusahau kipigo walichopata katika Derby della Madonnina dhidi ya wapinzani wao AC Milan.
Inter ilianza mchezo kwa kasi na kupata bao la kwanza dakika ya nane kupitia beki Yann Bisseck, aliyemalizia vizuri pasi ya Djed Spence kwa kupiga shuti lililojaa ufundi na kutinga kona ya chini ya lango. Wageni hao waliendelea kutawala mchezo na kutengeneza nafasi kadhaa kupitia Federico Dimarco na Marcus Thuram, huku kipa wa Feyenoord akifanya kazi ya ziada kuzuia mabao zaidi.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho bilakusahau michezo ya kasino mtandaoni. Bashiri kijanja hapa
Dakika ya 35, Inter iliongeza bao la pili kupitia mshambuliaji Francesco Pio Esposito, aliyefanikiwa kuunganisha kwa kichwa mpira uliotokana na shuti la Djed Spence lililokuwa limegongwa na mchezaji wa Feyenoord na kuelekea kwake. Feyenoord ilipata nafasi chache za kujibu, lakini kipa Josep Martinez alikuwa imara kuzuia juhudi za Anis Hadj Moussa kabla ya mapumziko.
Kipindi cha pili kilianza kwa Inter kuendelea kuonyesha ubora wake, ambapo dakika ya 54 Piotr Zielinski alifunga bao la tatu kwa shuti kali kutoka nje ya eneo la hatari lililogonga mwamba wa lango kabla ya kuingia wavuni. Esposito aliongeza bao jingine dakika za baadaye, lakini mwamuzi alilikataa baada ya kubainika kuwa mshambuliaji huyo alikuwa ameotea. Feyenoord ilijaribu kutafuta bao la kufutia machozi, lakini ilishindwa kupata nafasi kubwa za kuwatisha wageni hao.
Ushindi huo umeendeleza rekodi nzuri ya Inter dhidi ya timu za Uholanzi katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, ikiwa sasa haijapoteza katika michezo 14, ikishinda 11 na kutoka sare tatu. Aidha, Inter imepata ushindi wake wa pili katika mechi tano za ugenini za hivi karibuni kwenye michuano hiyo, baada ya kupoteza michezo mitatu. Kwa upande wa Feyenoord, kipigo hicho kimekuwa cha kwanza kwao wakiwa nyumbani msimu huu.


