Timu ya taifa ya Iran imewasili rasmi nchini Marekani kwa ajili ya kushiriki Kombe la Dunia 2026, huku ikipokelewa kwa shangwe na mashabiki waliojitokeza kwa wingi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Los Angeles jana Jumapili, Juni 14.
Wachezaji na benchi la ufundi la Iran walionekana kuwa katika hali nzuri walipowasili jijini humo kabla ya kuelekea hotelini walikofikia kwa ajili ya kuendelea na maandalizi ya mchezo wao wa kwanza wa michuano hiyo. “Tumefurahi kuona sapoti kubwa kutoka kwa mashabiki wetu, jambo linalotupa motisha kuelekea mechi ijayo,” amesema mmoja wa maofisa wa timu hiyo.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kabla ya kuingia Marekani, kikosi hicho kilikuwa kimeweka kambi katika mji wa Tijuana nchini Mexico, ambapo kilifanya mazoezi na maandalizi ya mwisho kwa ajili ya mashindano hayo makubwa zaidi ya soka duniani. Kambi hiyo ilitumika kuwapa wachezaji mazingira bora ya kujiandaa kabla ya kuanza rasmi safari yao ya michuano hii.
Iran iliondoka Tijuana kwa safari fupi ya ndege kuelekea Los Angeles, huku mashabiki waliokuwa nchini Mexico wakijitokeza kwa idadi kubwa kuwaaga na kuwapa maneno ya hamasa. “Tunawaamini na tunatarajia kuona wakifanya vizuri katika mashindano haya,” walinukuliwa baadhi ya mashabiki hao wakisema.
Sasa macho ya Wairan yanaelekezwa kwenye mchezo wao wa kwanza wa Kundi G dhidi ya New Zealand utakaochezwa kesho katika Uwanja wa Los Angeles. Kikosi hicho kina matumaini ya kuanza kampeni yake kwa matokeo mazuri na kuweka msingi imara wa kusaka nafasi ya kufuzu hatua ya mtoano.


