Iraola aahidi kuijenga Liverpool yenye kasi na mapambano

Kocha mpya wa Liverpool, Andoni Iraola, amesema anatamani kuijenga timu ambayo mashabiki watajivunia, huku akieleza kuwa msingi wa mafanikio yake utakuwa ni kufanya kazi kwa bidii, kucheza kwa kasi na kuwa na ushindani mkubwa. Iraola alitoa kauli hiyo katika mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari tangu achukue nafasi ya Arne Slot.

Iraola aahidi kuijenga Liverpool yenye kasi na mapambano“Nataka mashabiki wawe na timu ambayo wanaweza kujivunia. Tunataka kujulikana kwa kufanya kazi kwa bidii na kucheza kwa nguvu kubwa,” alisema Iraola.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 44 pia alifichua kuwa Liverpool inaendelea kufanya kazi kwa bidii kusajili wachezaji wapya kabla ya dirisha la usajili kufungwa, hasa baada ya kuondoka kwa baadhi ya wachezaji wenye uzoefu na wengine kusumbuliwa na majeraha. Aidha, alithibitisha kuwa Hugo Ekitike, Conor Bradley na Giovanni Leoni watakosekana mwanzoni mwa msimu kutokana na majeraha. “Kutakuwa na kipindi ambacho hatutakuwa nao. Tutalazimika kutafuta suluhisho la kuziba nafasi zao,” alieleza kocha huyo.

Iraola aahidi kuijenga Liverpool yenye kasi na mapambanoAkizungumzia kiungo Harvey Elliott, aliyerejea mapema kutoka kwa mkopo Aston Villa, Iraola alisema amevutiwa na ari aliyoionyesha mchezaji huyo na kuahidi kumpa nafasi ya kujidhihirisha katika maandalizi ya msimu mpya. Aliongeza kuwa msimu uliopita haukuwa rahisi kwa Elliott kutokana na mazingira yaliyomzuia kupata nafasi ya kucheza akiwa kwa mkopo.

Iraola aahidi kuijenga Liverpool yenye kasi na mapambano

“Harvey ameonyesha hamu kubwa ya kujithibitisha. Atapata nafasi katika maandalizi ya msimu na nina matumaini tutamuona akiwa katika kiwango kizuri. Pia nitabaki kuwa kocha yuleyule, kwa sababu lazima uwe wewe mwenyewe hata unapofundisha wachezaji wenye majina makubwa. Ratiba ya Liverpool ni changamoto kubwa, lakini pia ni fursa nzuri kwangu,” alisisitiza Iraola.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.