Iraola Aanza Kwa Kishindo Liverpool Ikiichapa Sunderland 4-2

Kocha mpya wa Liverpool, Andoni Iraola, ameanza rasmi maisha yake ndani ya klabu hiyo kwa ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Sunderland katika mchezo wa kirafiki wa maandalizi ya msimu mpya uliochezwa jijini Nashville, Marekani.

Iraola Aanza Kwa Kishindo Liverpool Ikiichapa Sunderland 4-2Liverpool ilionyesha kiwango kizuri katika mchezo huo kupitia mabao yaliyofungwa na Kieran Morrison, Dominik Szoboszlai, Federico Chiesa na Lewis Koumas, lakini furaha ya ushindi ilififishwa na jeraha la beki Joe Gomez, ambaye alitolewa nje ya uwanja ndani ya dakika 10 za mwanzo.

ligi kuu ya uingereza, ligi kuu England, odds za epl, mechi za ligi kuu uingereza, bashiri mechi za EPL, beti mechi za premier league, odds za ligi kuu England, odds za premier league

Iraola Aanza Kwa Kishindo Liverpool Ikiichapa Sunderland 4-2Baada ya mchezo, Iraola alisema bado kuna mambo mengi ya kuboresha kwani kikosi chake kinatoka kwenye kipindi kigumu cha mazoezi na wachezaji bado hawajafikia kiwango bora cha utimamu wa mwili.

Iraola Aanza Kwa Kishindo Liverpool Ikiichapa Sunderland 4-2Jeraha la Gomez limekuwa pigo la kwanza kwa Liverpool katika maandalizi ya msimu, baada ya klabu hiyo kufanikiwa kumaliza mazoezi ya awali bila kumpoteza mchezaji yeyote kutokana na majeraha.

“Bado tuna mambo mengi ya kurekebisha. Huu ulikuwa mchezo wetu wa kwanza na wachezaji walionekana kuwa na uchovu kutokana na mazoezi. Hata hivyo, huu ni mwanzo mzuri wa kujifunza na kuboresha. Habari mbaya zaidi ni jeraha la Joe Gomez, ambalo limetuumiza mapema kabisa,” amesema Iraola.

Iraola Aanza Kwa Kishindo Liverpool Ikiichapa Sunderland 4-2Kocha huyo Mhispania pia alizungumzia hali ya beki mpya Jeremy Jacquet, akieleza kuwa ataingizwa taratibu baada ya kukaa nje kwa muda mrefu kutokana na jeraha la bega. Liverpool itaendelea na ratiba yake ya mechi za kirafiki dhidi ya Wrexham, Leeds United, AS Monaco na Como, kabla ya kuanza kampeni ya Ligi Kuu England kwa mchezo wa ugenini dhidi ya Newcastle United Agosti 23.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.