Kocha wa Liverpool, Andoni Iraola, amesema kikosi chake bado kinahitaji kuongezewa nguvu katika dirisha la usajili kufuatia kuondoka kwa baadhi ya wachezaji muhimu pamoja na changamoto ya majeraha inayolikabili kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu England.
Liverpool tayari imewasajili Jeremy Jacquet na Victor Munoz, lakini imewapoteza Mohamed Salah, Andy Robertson na Ibrahima Konate. Aidha, Hugo Ekitike, Conor Bradley na Giovanni Leoni kwa sasa wako nje ya uwanja wakitumikia majeraha, hali inayoongeza pengo katika kikosi hicho.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kocha huyo raia wa Hispania alisema ni vigumu kutaja idadi kamili ya wachezaji wanaohitajika kwani soko la usajili bado linaendelea, huku akisisitiza kuwa klabu itaendelea kufuatilia fursa zitakazosaidia kuboresha kikosi bila kufanya maamuzi ya haraka.
“Kuna maeneo ambayo ni wazi tunahitaji kuongeza wachezaji. Kwa mfano, tunahitaji kabisa kumsajili winga. Pia yapo maeneo mengine ambayo tutayachambua kulingana na fursa zinazopatikana sokoni, gharama za usajili na kiwango cha wachezaji tulionao. Tuna baadhi ya nafasi ambazo zina changamoto kutokana na majeraha, ingawa bado tuna imani na wachezaji wetu,” alisema Iraola.
Iraola pia alisisitiza umuhimu wa kubaki kwa kipa Alisson Becker, ambaye mustakabali wake Anfield bado unaendelea kuzua mjadala. Kocha huyo alisema uzoefu wa Alisson, Virgil van Dijk na Joe Gomez utakuwa muhimu katika kuwasaidia wachezaji wapya na vijana kuzoea mazingira ya timu. Liverpool itaanza maandalizi ya msimu mpya kwa mchezo wa kirafiki dhidi ya Sunderland kabla ya kukutana na Wrexham, Leeds United, AS Monaco na Como, huku mechi yao ya kwanza ya Ligi Kuu England ikiwa dhidi ya Newcastle United Agosti 23.


