Klabu ya Newcastle United iko mbioni kukubaliana na klabu ya Real Sociedad kumsajili mchezaji wa timu hiyo Alexender Isak raia wa sweeden.

klabu ya Newcastle ipo kwenye mchakato wa kuitengeneza timu hiyo kua miongoni mwa timu tishio nchini Uingereza na hata Ulaya kwa ujumla,klabu ya Real Sociedad imekubaliana na klabu hiyo ya nchini Uingereza kwa ada ya uhamisho wa paundi milioni 58.

Newcastle, Isak Kutua Newcastle., Meridianbet

Nyota huyo wa zamani wa klabu ya klabu ya Borrusia Dortmund mwenye miaka 22 anakua mchezaji wa saba kusajiliwa kwa klabu hiyo katika majira haya ya joto.

klabu ya Newcastle ambayo ipo kwenye umiliki wa bilionea mpya kutoka falme za kiarabu wanaonekana kudhamiria kuijenga timu hiyo kuirudisha katika zama zake ikumbukwe Newcastle ilikua moja ya timu tishio nchini Uingereza kwenye miaka ya tisini.

Hivo kama matajiri hao kama watafanikisha dhamira yao hiyo basi watairudisha timu katika ubora wake iliokua nao miaka ya nyuma.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa