Kiungo wa Real Madrid Isco amethibitisha kwamba ataondoka Bernabeu kama mchezaji huru wakati wa dirisha hili la usajili na ilionekana anaweza kutimkia Uingereza ambako alikuwa akihusishwa na vilabu kama Chelsea, Arsenal na Tottenham.

Isco Athibitisha Kusepa Real Madrid

Isco alijiunga na Madrid mwaka 2013 akitokea Malaga mwaka 2013 kwa dau la £27m ambapo alifanikiwa kufunga mabao 53 katika michezo 353 kwenye mashidano yote ingawa amekuwa akipambania muda wakucheza miaka ya hivi karibuni akifanikwa kucheza michezo 14 akiwa na chini ya Ancelotti msimu huu wa Laliga.

Ripoti za awali zinaonyesha kwamba anaweza kuhamia Sevilla lakini hakuna kilichothibitishwa na klabu tatu za London bado zinaweza kurejesha nia yao. Wakati huo huo, Isco amewaaga Real Madrid kwa hisia.

“Baada ya Miaka tisa muda wangu katika klabu umeisha, jambo ambalo limeniwezesha kutimiza ndoto zangu zote nilipokuwa mdogo.

“Mbali na kutimiza ndoto, kushinda mataji mengi kuliko nilivyofikiria, kucheza na watu wakubwa zaidi, na kukutana na watu wa ajabu: NIMEKUWA NA WAKATI MZURI SANA BERNABEU.


SHINDA SAMSUNG A32 NA AVIATOR

SHINDA Samsung A32 ukiwa na mchezo wa Aviator kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet! Kwea pipa ukusanye zawadi zako pamoja na ushindi mnono wa mkwanja!

kasa wa njano, Kasa wa Njano Awapa Ubingwa wa CL Liverpool., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa