Timu ya taifa ya Italy (The Azzurri) ni mabingwa mara nne wa kombe la Dunia lakini mara ya mwisho kuwepo kwenye viwango vya juu FIFA ilikuwa ni Agosti 2016.

Walishindwa kufuzu kushiriki World Cup mwaka 2018 wakati wa utawala wa Gian Piero Ventura, lakini Roberto Mancini ambaye ametimiza umri wa miaka 56 siku ya Ijumaa, ameisuka tena timu hiyo na kuigeukia bahati yao.

Italy Imeingia Kwenye 10 Bora Baada ya Miaka Minne.
Kikosi cha timu ya taifa ya Italia katika michuano ya Nations League.

Italia ilikuwa nafasi ya 20 katika listi ya FIFA wakati Mancini anachukua mikoba ya kuwa kocha mkuu mwaka 2018, lakini sasa wameshinda michezo yao yote 10 ya kufuzu kushiriki Euro 2020.

Italia imefika fainali ya michuano ya Nations League na sasa wamefikisha idadi ya michezo 22 bila kupoteza rekodi bora tangu mwaka walishinda World Cup mwaka 2006.

Mancini amekisifu kikosi chake kwa jitihada walizoonesha mapema mwezi huu, alisema katika RAI Sport: “Wachezaji wamefanya kazi kubwa kwa sababu haijawahi kuwa rahisi.

“Tulijaribu kuwa wasumbufu sana na wachezaji wetu, unatakiwa kuwa na fikra sahihi kwaajili ya kuwa mzuri mtindo wa uchezaji kama zifanyavyo timu zote kubwa.

Italia imepanda kutoka nafasi ya 12 mpaka nafasi 10 katika listi mpya ya viwango ya FIFA wakati Mexico imepanda kwa nafasi mbili mpaka kufikia nafasi ya 9.

Kwa upande wa Mexico imechukua muda mrefu mpaka kuingia kwenye kumi bora baada ya kusota kwa miaka tisa tangu mara ya mwisho kuwepo katika kumi bora za FIFA.

Belgium imeendelea kubaki juu katika viwango vya FIFA mbele ya Ufaransa na Brazil.

Hii hapa 10 Bora ya FIFA: 1 Belgium, 2 France, 3 Brazil, 4 England, 5 Portugal, 6 Spain, 7 Argentina, 8 Uruguay, 9 Mexico, 10 Italy.


USICHELEWE KUKAMATA MKWANJA HUU!

Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.

Meridianbet Tanzania Casino

SOMA ZAIDI

16 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa