Raul Jimenez aliumia fuvu la kichwa na kufanyia upasuaji katika mchezo wa Jumapili dhidi ya Arsenal, Wolves iliposhinda 2-1,klabu imethibitisha.
Jimenez Apata Jeraha la Fuvu la Kichwa.
David Luiz na Raul Jimenez walipo gongana vichwa katika dimba la Emirates.

Jimenez aligongana vibaya na beki wa kati wa Arsenal David Luiz alipokuwa akizuia kona iliyopigwa dakika ya tano ya mchezo katika dimba la Emirates Stadium na kuondolewa uwanjani huku akiwa amewekwa mashine ya kusaidia kupumua.

Wolves wameuhabarisha uma siku ya Jumatatu, kwa kuthibitisha asili ya jeraha na kuongeza kuwa Mmexico huyo anaendelea vizuri baada ya upasuaji.

“Raul anaendelea vizuri baada ya kufanyiwa oparesheni usiku wa kuamkia leo ambao ulifanyika katika hosptali ya London,” Taarifa ya klabu ilisomeka hivyo.

“Kwa sasa amepumzika na yupo na mwenza wake Daniela na atabaki katika uchinguzi kwa siku cheche zijazo wakati akiendelea kujitizamia.

“Klabu inapenda kutoa shukrani kwa watumishi wa afya wa Arsenal, hospitali ya NHS na madokta waliyoshiriki kwenye operesheni kwa jitihada zao na ujuzi wao kwa kumsadia Jimenez.

Kocha wa Wolves Nunos Espirito Santo na kocha wa Arsenal walimtakia kheri Jimenez uopnywaji wa haraka baada ya mechi.

Wolves ambao walikuwa wageni katika dimba la Emirates wamesogea mapaka nafasi ya sita kwenye msimamo wa EPL baada ya kushinda mechi hiyo.


FURAHIA MUZIKI MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Mchezo wa Astro Legend unakupatia burudani ya muziki kupitia kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

Jimenez, Jimenez Apata Jeraha la Fuvu la Kichwa., Meridianbet

INGIA MCHEZONI

15 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa