Mshambuliaji wa Wolves Raul Jimenez ataruhusiwa kutoka hospitalini “mapema wiki ijayo” baada ya kuvunjika fuvu kwenye mchezo dhidi ya Arsenal Jumapili, klabu imethibitisha.

Jimenez alipata mgongano mkali wa vichwa na beki wa Arsenal David Luiz katika ushindi wa Wolves 2-1 dhidi ya Gunners.

Jimenez Kuruhusiwa Kutoka Hospitali Wiki Ijayo.

Tukio hilo la dakika ya tano lilimwacha Jimenez akihitaji matibabu kwenye uwanja kwa muda wa dakika 10 kabla ya kubebwa kwa machela.

Wakati David Luiz alikuwa na maamivu kichwani, Wolves ilifafanua asubuhi iliyofuata kwamba Jimenez alivunjika fuvu na akafanyiwa upasuaji.

Wolves hawakuweka wazi muda wa matibabu yake ingawa walithibitisha Alhamisi Meksiko huyo anapaswa kuwa nyumbani mapema wiki ijayo.

Taarifa iliyotolewa na daktari wa Wolves Matt Perry kwenye wavuti ya kilabu ilisomeka: “Kufuatia jeraha la Raul Jumapili, na upasuaji uliofuata, amekuwa akiendelea kujitizamia hospitalini.

“Tumefurahishwa na ripoti kutoka kwa mtaalamu wake; amefanya maendeleo mazuri. Anapaswa kuwa tayari kuondoka hospitalini mapema wiki ijayo.

“Raul na familia yake wanashukuru sana kwa faragha waliyopewa, na kwa msaada mkubwa ambao wamehisi kutoka kwa familia ya mpira wa miguu na kwingineko.

“Raul anashukuru sana kwa ujumbe wote wa nia njema anayoendelea kupokea, ambayo kwa hakika itamsaidia wakati wa kupona.”

Kwa vyovyote vile, Jimenez anaonekana amewekwa kwa kipindi kirefu na hiyo itakuwa pigo kubwa kwa Wolves.

Wolves ambayo ni ya saba kwenye jedwali la Premier League baada ya mechi 10 wanaweza kupanda katika msimaamo lakini itakuwa vita kubwa bila uwepo Jimenez.


FURAHIA MUZIKI MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Mchezo wa Astro Legend unakupatia burudani ya muziki kupitia kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

Jimenez, Jimenez Kuruhusiwa Kutoka Hospitali Wiki Ijayo., Meridianbet

INGIA MCHEZONI

29 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa