Mshambuliaji wa Chelsea, Joao Pedro, ameongeza mkataba wake na klabu hiyo utakaomuweka Stamford Bridge hadi mwaka 2034.Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, ambaye hakujumuishwa kwenye kikosi cha Brazil kwa ajili ya Kombe la Dunia la mwaka huu, alikuwa akihusishwa na interest kutoka kwa baadhi ya klabu kubwa barani Ulaya.
Pedro amesema amefurahia kupata nafasi ya kuendelea na safari yake Chelsea, akieleza kuwa kuchezea klabu kubwa imekuwa ndoto yake tangu akiwa mdogo.“Siku zote nimekuwa nikiota kuchezea klabu kubwa, na ina maana kubwa kwangu kutoa ahadi ya muda mrefu kwa klabu hii,” alisema Pedro.
Pedro aliongeza kuwa amekuwa na uhusiano mzuri na watu wote ndani ya Chelsea na amejisikia kama yupo nyumbani tangu alipowasili jijini London.“Nina uhusiano mzuri sana na kila mtu hapa klabuni, na nimejisikia kuwa nyumbani hapa London tangu siku nilipojiunga,” aliongeza.
Joao Pedro alijiunga na Chelsea akitokea Brighton mwaka jana na msimu uliopita alifunga mabao 20 katika mashindano yote. Chelsea inaanza kampeni yake ya Ligi Kuu England kwa mchezo dhidi ya Fulham siku ya Jumatatu.


