Timu ya taifa ya Canada imeendelea kuonyesha ubora wake kwenye michuano ya Dunia 2026 baada ya kuifunga Qatar mabao 6-0 katika mchezo wa Kundi B, huku mshambuliaji wake Jonathan David akiandika historia kwa kufunga hat-trick ya pili ya mashindano hayo.
David alikuwa nyota wa mchezo huo baada ya kufunga mabao matatu katika dakika za 29, 45+3 na 90+2, akiiwezesha Canada kupata ushindi mkubwa na kuongeza matumaini ya kufanya vizuri katika hatua ya makundi. “Jonathan David amejiunga na orodha ya wachezaji waliotikisa Kombe la Dunia kwa hat-trick zao,” ilielezwa baada ya mchezo huo.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Hat-trick hiyo imekuwa ya pili katika fainali za Dunia 2026 zinazoandaliwa kwa pamoja na Marekani, Canada na Mexico. Ya kwanza ilifungwa na Lionel Messi wakati Argentina ilipoibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Algeria katika moja ya michezo ya awali ya mashindano hayo.
Mbali na David, Canada ilipata mabao mengine kupitia kwa Cyle Larin aliyefunga dakika ya 16 na Nathan Saliba aliyetikisa nyavu dakika ya 64. Bao lingine lilitokana na Mohammad Al Mannai wa Qatar aliyejifunga dakika ya 75, jambo lililozidisha mateso kwa timu hiyo ya Mashariki ya Kati.
“Ulikuwa usiku maalumu kwa Canada na hasa Jonathan David,” walieleza wachambuzi wa mchezo baada ya filimbi ya mwisho. Ushindi huo mkubwa umeifanya Canada kujiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele huku Qatar ikiendelea kutafuta matokeo ya kuokoa kampeni yake kwenye michuano Dunia 2026.


