Juventus Waondoa Jersey ya Paulo Dybala sokoni

Klabu ya Juventus imeondoa Jersey ya Paulo Dybala kwenye maduka yake yote na nchini Italia lakini cha kushangaza kuwa jersey za Federico Bernardeschi, Giorgio Chiellini na Alvaro Morata hazikuondolewa sokoni.

Paulo Dybala anamalizia mkataba wake na klabu hiyo, baada ya hapo atakuwa huru kujiunga na klabu yoyote. Mchezaji huyo wa kimataifa kutokea Argentina ameshawaaga mashabiki wa klabu ya Juventus kwenye Dimba Allianz ambapo alimwaga machozi wakati anaaga.

Wachezaji ambao wataachwa na Juventus msimu huu kwenye majira ya kiangazi ni Morata, Bernardeschi na Chiellini, lakini Jersey zao bado zipo sokoni isipokuwa jersey ya Paulo Dybala.

Kwa sasa huwezi kuipata jersey namba 10 kwenye maduka ya klabu na mawakala wake, pia huwezi kuinunua jersey hio hata kwenye mtandao wa klabu.

Kuondoa jersey ya Paulo Dybala sokoni, kumezua maswali kwa mashabiki wa klabu ambapo kila mmoja maekuwa akizungumza lake kutoka na tukio hilo, hata walipotafutwa viongozi wa klabu ya Juventus hakuna aliyekuwa tayari kuzungumza.


ALIYA’S WISHES

Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA

Acha ujumbe